Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Kijana Songwe Amwaga Ujumbe Mzito: “Viongozi Msimfiche Ukweli Rais Samia”

November 25, 2025

DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

November 25, 2025

Tiba kwa wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa

November 25, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Kijana Songwe Amwaga Ujumbe Mzito: “Viongozi Msimfiche Ukweli Rais Samia”
  • DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA
  • Tiba kwa wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa
  • Waziri Mkuu Ajibu Maswali Mazito Toka kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari
  • WAZIRI NANAUKA ATAKA VIJANA WASIKILIZWE
  • Je, unatafuta kazi kwa muda mrefu fanya hivi
  • Waziri Mkuu aagiza Kanisa la Ufufuo na Uzima kufunguliwa
  • Kutoka hasara hadi faida katika biashara, mbinu ni hii
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA
Habari za Kitaifa

DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuNovember 25, 2025Updated:November 25, 2025No Comments2 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania ni mali ya Watanzania wote wala si ya Serikali au chama cha siasa na hivyo kila mmoja anapaswa kuilinda.

“Tanzania si mali ya Serikali, Tanzania si mali ya chama cha siasa na vyama vya siasa vipo kwa sababu nchi ipo. Tuilinde nchi yetu. Mungu ametupa nchi nzuri na kila mmoja ana wajibu wa kuilinda,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Novemba 25, 2025) wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Amesema fedha zinazotumika kujenga miundombinu ya barabara, zahanati, vituo vya afya, miradi ya maji ni za Watanzania na wala si za Serikali. “Hakuna fedha ya Serikali kwenye miradi. Fedha yote inayotekeleza miradi ni yako Mtanzania isipokuwa inasimamiwa na Serikali.”

Amesema kila Mtanzania anachangia pato la Taifa na anajinyima aina fulani ya maisha ili kujenga barabara au zahanati kwenye eneo lake. “Ukinunua shati kuna sehemu unapeleka kujenga barabara, unakuwa umetenga sehemu ya kutumia na sehemu umejinyima ili kuchangia maendeleo ya nchi.”

Akielezea madhara ya vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu, Waziri Mkuu amesema vitendo vile vililenga kuhujumu uchumi wa nchi na vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuchoma ofisi za serikali 756; vituo vya mabasi ya mwendokasi 27; mabasi sita; nyumba za watu binafsi 273; vituo vya polisi 159; vituo vya mafuta 672; magari ya watu binafsi 1,642; pikipiki 2,268; magari ya serikali 976 zikiwemo ambulance.

Amesema maisha ya Mtanzania mmojammoja yanahusisha mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kujipatia riziki zao. “Maisha ya Mtanzania ni ya kutoka eneo moja aende eneo jingine; haya si maisha ya Serikali, ni maisha ya Mtanzania mmoja mmoja. Maisha ya mwana Dar es Salaam ni kutoka hatua moja kwenda nyingine. Hakuna Mtanzania ambaye amejilimbikizia mali kwamba anaweza akakaa mwaka mzima bila kutoka. Atatoka Mbezi aende Posta, atatoka Kimara aende Kariakoo, atatoka Kariakoo aende Goba. Hawa watu wasipotoka unataka wale nini?”

Amesema uharibifu wa miundombinu uliofanyika ulilenga kuua uchumi wa nchi. “Kwamba mpango uliwekwa pasiwe na miundombinu ya hawa watu kusafiri. Je, watakula nini? Walipanga kuchoma stendi ya mabasi ya Magufuli, kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi na reli ya SGR. Hizi siyo mali za Serikali, ni mali za umma. Hivi unapochoma kituo cha DAWASCO kinachowapa maji safi na salama unataka hawa watu waishije?” alihoji Waziri Mkuu.

Dkt. Mwigulu amewasisitiza Watanzania wawe mstari wa mbele kuilinda Tanzania kwa kutoa taarifa pale wanapobaini watu wasiofahamika kwani hivi sasa hawafikii kwenye nyumba za kulala wageni.

“Niwaelekeze viongozi wa Serikali ngazi zote kuanzia wa mitaa, kitongoji na wa kijiji wawe macho; hawa watu wabaya wabaya hawafikii tena kwenye nyumba za wageni, wanafikia kwa mtu mmoja mmoja. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, kwa kujua kuwa huyo aliyemleta ni nani.”

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema wale wasioitakia mema Tanzania wanatamani mabaya zaidi yaendelee kutokea, hivyo ni busara kuwakataa kwa kuwa wana dhamira ya kufanya uovu dhidi ya Tanzania. “Natamani kila mmoja alibebe jambo hili kwa ukubwa, hawa watu hawatupendi, wanaangalia rasilimali zetu. Tukumbuke kuwa nchi yetu siyo masikini, kuna watu wanamezea mate rasilimali zetu. Ninawahakikishia kuwa tutailinda Tanzania na rasilimali zake kwa gharama yoyote ile, watameza mate hadi yataisha,” amesisitiza.

Amesema kuwa watumishi wa umma wanapaswa kubadilisha mtazamo kuhusu sekta, kuiheshimu na kuacha kuwaona walioko kwenye sekta hiyo ni watu wa chini. “Hatutaushinda umasikini kama tutaamini kwamba sekta binafsi ni maadui, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amebadilisha sheria inayomruhusu mkandarasi mzawa apate mradi mkubwa na wale wakubwa waombe sub-contract kwake, hili litatengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wa Kitanzania,” amesisitiza Dkt. Mwigulu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja viongozi wa Jukwaa la Wahariri.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

WAZIRI NANAUKA ATAKA VIJANA WASIKILIZWE

November 25, 2025

RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA

November 22, 2025

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE

November 21, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025234

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024201

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025127
Don't Miss
Video Mpya

Kijana Songwe Amwaga Ujumbe Mzito: “Viongozi Msimfiche Ukweli Rais Samia”

By Mbeya YetuNovember 25, 20252

DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

November 25, 2025

Tiba kwa wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa

November 25, 2025

Waziri Mkuu Ajibu Maswali Mazito Toka kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari

November 25, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Kijana Songwe Amwaga Ujumbe Mzito: “Viongozi Msimfiche Ukweli Rais Samia”

November 25, 2025

DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

November 25, 2025

Tiba kwa wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa

November 25, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025234

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024201
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.