Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100

February 28, 2026

Mwalupindi Akabidhi Tuzo Vitabu na kufuturisha wanafunzi Kuimarisha Elimu Sangu Sekondari

February 28, 2026

VIONGOZI WA KIDINI,MAKUNDI YA KIJAMII WAPEWA SEMINA SAPOTI YA KISAIKOLOJIA KWA JAMII

February 28, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100
  • Mwalupindi Akabidhi Tuzo Vitabu na kufuturisha wanafunzi Kuimarisha Elimu Sangu Sekondari
  • VIONGOZI WA KIDINI,MAKUNDI YA KIJAMII WAPEWA SEMINA SAPOTI YA KISAIKOLOJIA KWA JAMII
  • TAKUKURU MBEYA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 100, YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
  • Mfumo wa kidigitali wa Vyeti vya Uasili kupitia Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) waanza rasmi Machi 2, 2026
  • MAHUNDI: SERIKALI KUIMARISHA ELIMU YA MALEZI KUPITIA KAMPASI YA KISANGARA
  • Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na NHIF Mkoa wa Mbeya waelimisha walemavu kuhusu Bima ya Afya
  • Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » Mhe. Mahundi: Wazee ni Tunu ya Taifa, Wastahili Kulindwa na Kuheshimiwa
Video Mpya

Mhe. Mahundi: Wazee ni Tunu ya Taifa, Wastahili Kulindwa na Kuheshimiwa

Mbeya YetuBy Mbeya YetuDecember 29, 2025No Comments6 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Wazee wanaoishi katika Makazi ya Wazee na wasiojiweza Bukumbi, wilayani Misungwi mkoani Mwanza, wameishukuru Serikali kwa kuimarisha huduma za ustawi wao, wakisema hatua hiyo imeleta faraja, heshima na matumaini mapya katika maisha yao ya uzeeni.

Mwenyekiti wa Wazee kituoni hapo, Mzee John Nguku amesema wazee wanathamini jitihada Serikali za kuwapatia huduma muhimu kwa wakati.

“Kwa niaba ya wazee wenzangu, tunaishukuru Serikali kwa kutukumbuka tunaishi kwa amani, tunahudumiwa kwa heshima na tunahisi bado tuna thamani katika jamii, tunaomba uangalizi huu uendelee ili wazee wengi zaidi wanufaike maana uzee siyo mzigo bali ni neema”. amesema Mzee John

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesema Serikali inawatambua wazee kama tunu muhimu ya Taifa na itaendelea kuimarisha huduma za ustawi na ulinzi wao.

Mhe. Mahundi amesema pamoja na jitihada za Serikali, jamii ina wajibu wa msingi wa kuwatunza wazee, huku akiwataka vijana kutowasahau wazazi wao wanapofikia uzee na kuhakikisha wanapata upendo, heshima na msaada unaostahili.

“Nawasihi vijana na jamii kwa ujumla, msije mkawasahau wazazi wenu wanapofikia uzee. Kuwatunza wazee ni wajibu wa familia na ni sehemu ya maadili yetu ya Kitanzania, Serikali itaendelea kuhakikisha wazee wanathaminiwa, wanalindwa na wanapata huduma stahiki bila kubaguliwa. Tunazitaka familia, vijana na jamii kwa ujumla kutambua kuwa kuwajali wazee ni wajibu wa kimaadili na msingi wa ustawi wa Taifa letu” amesema Mhe. Mahundi.

Kwa upande wake, Mfawidhi wa Makazi ya Wazee na wasiojiweza Bukumbi, Vivian Kaiza amesema uangalizi wa Serikali na ushirikiano wa wadau umeendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa wazee waliopo kituoni hapo, Makazi yanaendelea kusimamiwa kwa weledi na kujali maslahi ya wazee, huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha wazee wanapata huduma stahiki na kuishi kwa amani.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya Serikali katika kuimarisha ustawi wa wazee, huku jamii ikihimizwa kushirikiana na Serikali katika kuwatunza wazee ili waishi maisha yenye heshima, upendo na matumaini.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VIONGOZI WA KIDINI,MAKUNDI YA KIJAMII WAPEWA SEMINA SAPOTI YA KISAIKOLOJIA KWA JAMII

February 28, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na NHIF Mkoa wa Mbeya waelimisha walemavu kuhusu Bima ya Afya

February 25, 2026

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

February 22, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025361

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025253

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss
Habari za Kitaifa

SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100

By Mbeya YetuFebruary 28, 202613

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mzee Rashidi Mfaume Kawawa, mwanasiasa mashuhuri na…

Mwalupindi Akabidhi Tuzo Vitabu na kufuturisha wanafunzi Kuimarisha Elimu Sangu Sekondari

February 28, 2026

VIONGOZI WA KIDINI,MAKUNDI YA KIJAMII WAPEWA SEMINA SAPOTI YA KISAIKOLOJIA KWA JAMII

February 28, 2026

TAKUKURU MBEYA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 100, YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

February 27, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100

February 28, 2026

Mwalupindi Akabidhi Tuzo Vitabu na kufuturisha wanafunzi Kuimarisha Elimu Sangu Sekondari

February 28, 2026

VIONGOZI WA KIDINI,MAKUNDI YA KIJAMII WAPEWA SEMINA SAPOTI YA KISAIKOLOJIA KWA JAMII

February 28, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025361

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025253

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.