Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

February 22, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026

DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI

February 21, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO
  • NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.
  • DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI
  • TAZAMA DKT TULIA NA DKT. MARY MWANJELWA WAKIIMBA WIMBO WA Umbili
  • UTANI WA DKT. TULIA ACKSON WAACHA HISIA NZITO MAZISHI YA MWANAHABARI MKONGWE ULIMBOKA MWAKILILI
  • MAHUNDI ASEMA SERIKALI INAWATHAMINI WAZEE KAMA HAZINA YA HEKIMA NA MAADILI YA TAIFA
  • SUMA FYANDOMO MGENI RASMI BARAZA LA WANAWAKE (UWT) RUNGWE AWASHUKURU KWA MSHIKAMANO
  • MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.
Habari za Kitaifa

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

Mbeya YetuBy Mbeya YetuFebruary 22, 2026No Comments3 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasihi watu wenye uwezo kuwatunza wazazi na ndugu ili kuenzi mchango wao katika jamii.

Mhandisi Mahundi amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea makazi ya wazee yanayomilikiwa na taasisi binafsi ya Tushikamane Pamoja Foundation,Kwembe, Manispaa ya Ubungo Jijini Dar Es Salaam ambapo amesema jamii inapaswa kubadili mtazamo na kuhakikisha wazee wanapewa upendo, ulinzi na matunzo wanayostahili bila kujali changamoto zilizopita.

Ameeleza kwamba hata kama walipitia changamoto au walikosewa, ni muhimu kulipa kwa wema na si kwa mabaya, kwa sababu wazee ni tunu ya taifa na wana mchango mkubwa katika malezi na ujenzi wa jamii yetu.
Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wanaojitoa kuwahudumia wazee ili kuhakikisha wanapata huduma stahiki na wanaendelea kuishi kwa heshima na usalama,

Awali, akisoma taarifa fupi ya kituo hicho Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dkt. Aristides Raphael, , amesema Serikali imekuwa ikishirikiana kwa karibu na uongozi wa makazi hayo ambapo imefanikisha kuwapatia wazee wote bima za afya, Afisa Ustawi wa Jamii anayefika kituoni hapo mara mbili kwa wiki kwa ajili ya uangalizi na ushauri, pamoja na madaktari wanaotoa huduma za matibabu na huduma nyingine muhimu.

“Ushirikiano huu umewezesha wazee hawa kupata huduma muhimu ikiwemo matibabu, ufuatiliaji wa afya zao pamoja na ushauri wa kijamii, jambo ambalo limechangia kuboresha hali yao ya maisha na kuwafanya waishi kwa matumaini na utulivu zaidi,” amesema Dkt. Aristides.

Kwa upande wao, baadhi ya wazee wanaoishi katika makazi hayo wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwajali na kuthamini ustawi wao
wakieleza kuwa ujio wa viongozi na misaada mbalimbali imekuwa faraja kubwa kwao na uthibitisho kuwa bado wanatambuliwa na kuthaminiwa katika jamii.

“Tunashukuru Serikali na wadau mbalimbali kwa kuendelea kutupa faraja na kututembelea. Hii inatupa furaha kubwa na kutufanya tuone bado tuna thamani katika jamii. Tunaamini kweli kuwa wazee ni tunu ya Taifa na tunaomba juhudi hizi ziendelee ili kuwasaidia hata wazee wengine wenye uhitaji,” amesema mmoja wa wazee hao.

Makazi hayo yamekuwa yakitoa huduma za malezi, malazi na uangalizi kwa wazee wenye uhitaji, huku Serikali ikiendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kundi hilo linapata haki, heshima na ustawi unaostahili.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MAHUNDI ASEMA SERIKALI INAWATHAMINI WAZEE KAMA HAZINA YA HEKIMA NA MAADILI YA TAIFA

February 20, 2026

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

February 19, 2026

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025349

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024234

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss
Video Mpya

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

By Mbeya YetuFebruary 22, 20260

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026

DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI

February 21, 2026

TAZAMA DKT TULIA NA DKT. MARY MWANJELWA WAKIIMBA WIMBO WA Umbili

February 21, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

February 22, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026

DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI

February 21, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025349

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024234
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.