Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza

March 6, 2026

Mbunge CCM,wapinzani waimarisha umoja,wajadili maendeleo ya wana Mbeya

March 5, 2026

Dkt. Tulia Aunga Mkono Ujenzi wa Barabara Bombambili kwa Mifuko 100 ya Saruji na tripu 10 za mawe

March 5, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza
  • Mbunge CCM,wapinzani waimarisha umoja,wajadili maendeleo ya wana Mbeya
  • Dkt. Tulia Aunga Mkono Ujenzi wa Barabara Bombambili kwa Mifuko 100 ya Saruji na tripu 10 za mawe
  • SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100
  • Mwalupindi Akabidhi Tuzo Vitabu na kufuturisha wanafunzi Kuimarisha Elimu Sangu Sekondari
  • VIONGOZI WA KIDINI,MAKUNDI YA KIJAMII WAPEWA SEMINA SAPOTI YA KISAIKOLOJIA KWA JAMII
  • TAKUKURU MBEYA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 100, YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
  • Mfumo wa kidigitali wa Vyeti vya Uasili kupitia Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) waanza rasmi Machi 2, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza
Habari za Kitaifa

Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMarch 6, 2026No Comments5 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Dar es Salaam-Wakinamama waliolazwa katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Sinza jijini Dar es Salaam wamepatiwa msaada wa Comfy Mum pants uliotolewa na kampuni ya Comfy Mum kwa kushirikiana na Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC), ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani na kuonyesha upendo na kujali afya ya wanawake katika jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Comfy Mum, Bi. Irene Mville alisema kampuni hiyo imeona umuhimu wa kushiriki katika kuunga mkono wanawake, hususan waliotoka kujifungua na wanaokabiliwa na changamoto ya hedhi nyingi.

“Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Comfy Mum tumeona ni vyema kuwafikia wanawake waliopo hospitalini na kuwapatia mahitaji haya muhimu ili kuwafariji na kuwapa faraja katika kipindi hiki,” alisema Bi. Mville.

Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu wa TNCC, Bi. Judith Sarakikya, alisema ushirikiano huo unaonyesha dhamira ya sekta binafsi kushiriki katika kuimarisha ustawi wa wanawake.

“TNCC tunaamini kuwa kumwezesha mwanamke kunahusisha pia kujali afya na ustawi wake, ushirikiano huu na Comfy Mum unaonyesha namna sekta binafsi inavyoweza kushiriki kusaidia jamii,” alisema Sarakikya.

Naye Afisa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Sinza, Bi. Judith Katemba, aliishukuru Comfy Mum na TNCC kwa msaada huo akisema utasaidia kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini.

“Tunawashukuru sana Comfy Mum na TNCC kwa kutukumbuka. Msaada huu ni muhimu kwa wagonjwa wetu na unaonyesha kuwa jamii inaendelea kuwajali wanawake hata wanapokuwa kwenye changamoto za kiafya,” alisema Katemba.

Aliongeza kuwa hatua hiyo inaakisi mshikamano wa kijamii na kuthibitisha umuhimu wa ushirikiano katika kuunga mkono wanawake hususan katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Mbunge CCM,wapinzani waimarisha umoja,wajadili maendeleo ya wana Mbeya

March 5, 2026

SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100

February 28, 2026

TAKUKURU MBEYA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 100, YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

February 27, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025362

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025253

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025141
Don't Miss
Habari za Kitaifa

Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza

By Mbeya YetuMarch 6, 20265

Dar es Salaam-Wakinamama waliolazwa katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Sinza jijini Dar es…

Mbunge CCM,wapinzani waimarisha umoja,wajadili maendeleo ya wana Mbeya

March 5, 2026

Dkt. Tulia Aunga Mkono Ujenzi wa Barabara Bombambili kwa Mifuko 100 ya Saruji na tripu 10 za mawe

March 5, 2026

SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100

February 28, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza

March 6, 2026

Mbunge CCM,wapinzani waimarisha umoja,wajadili maendeleo ya wana Mbeya

March 5, 2026

Dkt. Tulia Aunga Mkono Ujenzi wa Barabara Bombambili kwa Mifuko 100 ya Saruji na tripu 10 za mawe

March 5, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025362

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025253

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.