Sheikh mkuu wa mkoa wa Mbeya Mohamed Mwansasu amewataka viongozi wa BAKWATA wajipambanue kwa Waislamu na kuweka bayana utendaji wao ili kuepusha Baraza hilo kuchukiwa na Waislamu.
Sheikh Mwansasu amebainisha kuwa upo mtafaruku baina ya Baraza hilo na Taasisi nyingine za Kiislamu na kuwa hiyo imetokana na baadhi ya viongozi ndani ya Baraza kujiona wao ndio BAKWATA.