#MbeyaYetuTv #TRA_Songwe #TRA_Mbeya
Watu Watano wamefariki dunia kutokana na ajali ya gari aina ya Landcruiser yenye nambari za Usajili STL 8825 Mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ambalo liligonga Lori aina ya FUSO yenye nambari za usajili T 586 ANE.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Hanseketwa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe majira ya saa 11 alfajiri leo Agosti 23,2021.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Meneja Msaidizi Forodha Mkoa Songwe Omar Mzava amewataja marehemu kuwa ni Bernad Mushingi,ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Tunduma,Azaria Sivonike (Dereva wa Gari),Joel Mitondwa,Said Budi na Fahad Hassan wote wakiwa ni Wafanyakazi kituo cha Mbeya.
Trending
- Kutoka kusota hadi usukani wenye utajiri
- Ikulu Dodoma: Rais Samia Azungumza na Mawaziri Baada ya Kuwaapisha
- Alivyokabiliana na changamoto ya ukosefu wa hamu ya tendo hadi kuishinda
- DKT. MWIGULU AKABIDHIWA OFISI RASMI
- Dkt. Tulia Aingia Uyole Kwa Kasi ya Moto: Afufua Makazi ya Mzee Aliyepata Janga la Moto
- Safari ya Uponyaji Kutoka katika Maumivu ya Hedhi
- RAIS SAMIA atangaza Baraza lake jipya la mawaziri
- Aondokana na umaskini wa kutupwa baada ya kujua mbinu za betting
