#MbeyaYetuTv #TRA_Songwe #TRA_Mbeya
Watu Watano wamefariki dunia kutokana na ajali ya gari aina ya Landcruiser yenye nambari za Usajili STL 8825 Mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ambalo liligonga Lori aina ya FUSO yenye nambari za usajili T 586 ANE.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Hanseketwa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe majira ya saa 11 alfajiri leo Agosti 23,2021.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Meneja Msaidizi Forodha Mkoa Songwe Omar Mzava amewataja marehemu kuwa ni Bernad Mushingi,ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Tunduma,Azaria Sivonike (Dereva wa Gari),Joel Mitondwa,Said Budi na Fahad Hassan wote wakiwa ni Wafanyakazi kituo cha Mbeya.
Trending
- SIRI YA UTAJIRI WA MWALUNENGE HII HAPA AWEKA BAYANA HAJATUMIA UGANGA WA MIUJIZA
- MSAADA WA DKT. TULIA WAFUTA MACHOZI YA FAMILIA YA BI. LUSIA KAPANGALA
- BONANZA LA NMB MWALIMU SPESHO MBEYA VIBE LAKE LACHANGAMSHA WALIMU JIJINI MBEYA
- Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
- ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA
- MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI
- KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO
- MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI