AJIUA KWA KUJICHOMA MOTO.Mnamo tarehe 08.11.2021 majira ya saa 03:00 asubuhi huko Kijiji cha Ihombekilichopo Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya MbeyaVijijini, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MASHAKA SAIMON @YOKONIA [35] Mkazi wa Kijiji cha Ihombe alikutwa ndani ya nyumba yakeakiwa amefariki dunia kwa kuungua moto.
Ni kwamba kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwamuda mrefu na alitelekezwa na mke wake hali iliyopelekea kukata tamaa yamaisha na siku chache zilizopita alifanya jaribio la kujilipua kwa Petrol kabla yakuokolewa na mdogo wake. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.Aidha ninatoa wito kwa wananchi/jamii kwa ujumla kutoa taarifa za mtu/watuwenye hali ya kukata tamaa ya Maisha kwa viongozi wao wa vijiji, mitaa kabla yakutokea madhara makubwa kama ilivyotokea kwa marehemu MASHAKASAIMON @ YOKONIA
Trending
- Baada ya hapo ndipo akapata kazi kubwa zaidi!
- SIMBACHAWENE ATEMBEA MITAANI KUANGALIA USALAMA—AWAPA HONGERA WANANCHI KWA UTULIVU
- Taarifa nyingine Tena Toka jeshi la polisi
- 2021 11 26 14 36 44
- SHILINGI BILIONI 6.7 KUTIBU WAGONJWA 760 WASIO NA UWEZO WA KUMUDU GHARAMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA
- Polepole hisia zilianza kurejea na maisha yalianza upya!
- Jeshi la Polisi latoa Taarifa muda huu
- Hali shwari Jiji la Mbeya
