Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilikataliwa na Wanaume Wote Lakini Hatua Niliyopiga Ilinifanya Niolewe na Tajiri

September 17, 2025

Aibu!! Askofu Mkuu abainika kuiba fedha kanisa lake

September 17, 2025

Kongamano la Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050 Kufanyika Mbeya

September 17, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilikataliwa na Wanaume Wote Lakini Hatua Niliyopiga Ilinifanya Niolewe na Tajiri
  • Aibu!! Askofu Mkuu abainika kuiba fedha kanisa lake
  • Kongamano la Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050 Kufanyika Mbeya
  • Prof. Makulilo: Watanzania Wajiandae kwa Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050
  • Tajiri wa madini aliyefilisika arejea tena katika biashara kwa kishindo
  • Nilirogwa Nipoteze Kila Kitu ila Hatua Niliyopiga Ilinivunja Minyororo Ya Uchawi
  • Niliibiwa Gari Yangu Usiku, Lakini Hatua Niliyopiga Ilifanya Wezi Wenyewe Walirudishe Hadi Getini
  • Nilipoteza Mume Wangu Kwa Mpango wa Kando ila Kitu Nilichojaribu Kilimfanya Aombe Radhi Hadharani
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » KAMATI YA SIASA CCM WILAYA YA MBEYA YATEMBELEA UWANJA WA KIMATAIFA SONGWE YASIFU UTEKELEZAJI ILANI
Video Mpya

KAMATI YA SIASA CCM WILAYA YA MBEYA YATEMBELEA UWANJA WA KIMATAIFA SONGWE YASIFU UTEKELEZAJI ILANI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuDecember 22, 2022No Comments1 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

#MbeyaYetuTv
Serikali inaendelea kujenga jengo kubwa la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe (SIA) uliopo katika kata ya Bonde la Songwe jimbo la Mbeya vijijini ikiwa ni mkakati wake wa kuboresha sekta ya usafiri wa anga ikiwemo kuweka mazingira rafiki kabla na baada ya abiria kusafiri kutoka na kwenda nchi mbalimbali.

Akitoa taarifa kwa kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbeya vijijini (Kichama) kwenye ukaguzi wa mradi huo Kaimu Meneja wa wakala wa barabara Tanzania TANROADS Mhandisi Joel Samwel Mwabungu alisema ujenzi huo unatekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 14 na wanatarajia kukamilisha jengo hilo kufikia march 2023.

Kuhusu uwekaji taa za kuongozea ndege kiongozi huyo alisema tayari zilishakamilika na zinatumika vizuri hivyo ndege zinaweza kutua na kuanza safari usiku na mchana.

Wajumbe wa kamati ya siasa akiwemo Danieli Kapusi, Willium Simwali na Subiraga Mwangoka walieleza kuridhishwa kwao na utekelezwaji miradi mbalimbali kwenye uwanja huo katika kupanua wigo wa kuwahudumia wasafiri.

Michael Ngailo ni Diwani wa Kata ya Bonde la Songwe ulipo uwanja wa ndege wa Songwe alisema uwanja huo umekuwa na faida kwa jamii isipokuwa changamoto ni wanafunzi wa eneo la Iwejele kuzuiliwa kupita kwenye eneo la uwanja kwenda shuleni baada ya mamlaka kujenga uzio kuzunguka uwanja huo na kuiomba serikali kupitia wizara ya uchukuzi kutekeleza ahadi zao kwa wananchi wa Kata ya Bonde la Songwe Mbeya vijijini.

Msafara wa Kamati ya siasa uliongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Sebastian Mwalupindi ambapo baada ya kamati kukagua mfumo wa taa za kuongozea ndege uwanjani hapo na baadaye kukagua jengo la abiria alisema utekelezaji wa ilani ya chama hicho ni wa kiwango cha juu na kinachoridhisha.

Pamoja na hayo CCM wilaya ya Mbeya vijijini kupitia Mwenyekiti Mwalupindi imetumia ziara hiyo ya kikazi kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Mwenyekiti wa Chama (CCM) Taifa katika uchaguzi wa hivi karibuni.

Pia imempongeza Rais Samia kwa kuendelea kusimamia ipasavyo utekelezwaji miradi mbalimbali nchini katika kuwatumikia wananchi hususani katika sekta za miundombinu ya usafiri, Maji, Afya, Kilimo na Elimu.

Jengo hilo la abiria linajengwa kwa thamani kwa zaidi ya shilingi bilioni 14 na kampuni ya Kichina ambapo pamoja na miradi mingine ya uwanja wa ndege ya Run Ways na taa za kuongozea ndege jumla yake ni zaidi ya shilingi bilioni 30 zitakazotumika katika miradi hiyo.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Kongamano la Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050 Kufanyika Mbeya

September 17, 2025

BRANDY NELSON:’NILIUKOSA UDIWANI V/MAALUM 2020 NIKAANZA UPYA 2025 CHAMA KIMENICHAGUA KUGOMBEA KATA’

September 16, 2025

Mwalunenge Aunguruma Kata ya Iganzo: Asema Oktoba Ni Kazi Moja tu – Rais, Mbunge na Madiwani CCM

September 15, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025209

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024184

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025126

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025125
Don't Miss
Uncategorized

Nilikataliwa na Wanaume Wote Lakini Hatua Niliyopiga Ilinifanya Niolewe na Tajiri

By Mbeya YetuSeptember 17, 20251

Baadhi yao waliniambia waziwazi kuwa hawawezi kuwa na mwanamke mwenye ulemavu. Nilipita katika aibu nyingi…

Aibu!! Askofu Mkuu abainika kuiba fedha kanisa lake

September 17, 2025

Kongamano la Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050 Kufanyika Mbeya

September 17, 2025

Prof. Makulilo: Watanzania Wajiandae kwa Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050

September 17, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilikataliwa na Wanaume Wote Lakini Hatua Niliyopiga Ilinifanya Niolewe na Tajiri

September 17, 2025

Aibu!! Askofu Mkuu abainika kuiba fedha kanisa lake

September 17, 2025

Kongamano la Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050 Kufanyika Mbeya

September 17, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025209

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024184

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025126
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.