Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

February 19, 2026

Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ashiriki kampeni ya kitaifa ya uwekezaji wa ndani.

February 18, 2026

MBEYA YAANDIKA HISTORIA: NGazi ZA UMEME ZA KWANZA NYANDA ZA JUU KUSINI

February 18, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE
  • Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ashiriki kampeni ya kitaifa ya uwekezaji wa ndani.
  • MBEYA YAANDIKA HISTORIA: NGazi ZA UMEME ZA KWANZA NYANDA ZA JUU KUSINI
  • ZIMAMOTO WAOPOA MWILI WA KIJANA ALIYEDAIWA KUWA MWANAFUNZI WA CBE MBEYA
  • Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya
  • TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA
  • AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
  • SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » DARAJA LA MINYUGHE, WILAYANI IKUNGI, SINGIDA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI
Habari za Kitaifa

DARAJA LA MINYUGHE, WILAYANI IKUNGI, SINGIDA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMarch 24, 2024No Comments13 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Serikali imekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Minyughe na Makilawa, katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, lililokatika miaka mitatu iliyopita, na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu. Kukamilika kwa daraja hilo la chuma (Mibey Bridge) lenye urefu wa mita 30 lililogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.6/-katika barabara ya Mtamaa-Minyughe hadi Mtavira, Wilayani Ikungi, litaenda kufungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa kata hızo.Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Singida, Mhandisi Ibrahim Kibasa, alisema kukamilisha uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya daraja hilo, kumewezesha mto Minyughe kufunguka, na hivyo kutoa fursa kwa shughuli za uchukuzi kuendelea kati ya maeneo ya vijijini na makao makuu ya mkoa.Mhandisi Kibasa alisema kuwa, sasa wananchi wa kata tatu zinazounganishwa na daraja hilo, wataweza kuzikabili changamoto mbalimbali, zilizokwamisha shughuli zao, hususani wakati wa masika, kutokana na mto kufurika maji, kiasi cha kutishia usalama wao wakati wa kuvuka.

Ikungi

Serikali imekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Minyughe na Makilawa, katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, lililokatika miaka mitatu iliyopita, na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu.

Kukamilika kwa daraja hilo la chuma (Mibey Bridge) lenye urefu wa mita 30 lililogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.6/-katika barabara ya Mtamaa-Minyughe hadi Mtavira, Wilayani Ikungi, litaenda kufungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa kata hızo.

Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Singida, Mhandisi Ibrahim Kibasa, alisema kukamilisha uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya daraja hilo, kumewezesha mto Minyughe kufunguka, na hivyo kutoa fursa kwa shughuli za uchukuzi kuendelea kati ya maeneo ya vijijini na makao makuu ya mkoa.

Mhandisi Kibasa alisema kuwa, sasa wananchi wa kata tatu zinazounganishwa na daraja hilo, wataweza kuzikabili changamoto mbalimbali, zilizokwamisha shughuli zao, hususani wakati wa masika, kutokana na mto kufurika maji, kiasi cha kutishia usalama wao wakati wa kuvuka.

” Sehemu ya fedha hizo ni bajeti mwaka ya mwaka huu ambapo tumejenga madaraja ikiwemo daraja hili la Minyughe,daraja hili limekuwa likiwasumbua wananchi takribani miaka mitatu na hivyo kukwamisha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Kata tatu pamoja na Mkoa wa jirani wa Tabora, katika wilaya ya Uyui, inayopakana na wilaya hii ya Ikungi, “alisema.
**
Aidha, Mhandisi Kibasa alisema, ujenzi wa daraja hilo umetokana na bajeti ya mwaka iliyotengwa, kiasi cha Sh. Bilioni 4.4/- katika wilaya ya Ikungi kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja, katika halmashauri ya Wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia kukamilika kwa kazi hiyo, akiwemo Bi. Elizabeth Bakari wa Kijiji cha Minyughe, na diwani wa Kata Minyughe , Mhe. Nelson Kiwesi, waliishukuru Serikali kwa mradi huo, ambao baada ya kukamilika, unakwenda kuondoa adha ya usafiri, hasa kwa wajawazito.

Bi. Elizabeth alibainisha kuwa, iliwalazimu kukosa huduma muhimu ikiwemo zile za afya katika kituo cha afya kilichopo ng’ambo ya pili, pia watoto wao kuhatarisha maisha wakati wa kwenda shule na kurudi nyumbani, hususani nyakati za masika, kutokana na mto Minyughe kufurika maji.

Alisema kukamilika kwa daraja hilo, sasa watoto wao hawatakosa masomo, wajawazito na wagonjwa wataenda kupata Huduma za matibabu kwenye kituo cha afya kilichopo ng’ambo ya daraja hilo pamoja na kufungua shughuli za usafirishaji wa mazao na watu.

“Kujengwa kwa daraja hili, ni mafanikio makubwa kwa watoto wetu waliolazimika kushindwa kuhudhuria vipindi vya masomo yao darasani. Serikali itaongeza mapato kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi , ikiwemo kilimo, na mali asili kupitia misitu, wazalishaji wamerahisishiwa mawasiliano kati ya upande mmoja na ule wa pili,” alisema.

Awali Mhandisi Mshauri Ebenezer Mollel, kutoka TARURA makao makuu, kitengo cha madaraja, alisema daraja hilo ni la tatu kujengwa hapa nchini, likitanguliwa na mengine lililopo Kihansi, huko Kilombero na lile la Mbuchi, kule Kibiti, mkoani Pwani.

Mhandisi Mollel alisema kuwa, madaraja hayo ni ya aina ya kipekee, hivyo kabla ya ujenzi hulazimika kuwapatia mafunzo Wahandisi wa TARURA na TANROADS, lengo likiwa kuwajengea uwezo, kwa ajili ya kupata ujuzi na utaalamu zaidi kuweza kumudu majukumu yao, kulingana na kukua kwa teknolojia, huku wahandisi walioshiriki mafunzo hayo, wakifikia 42.

Kwa mujibu wa mhandisi Mollel, teknolojia ya daraja hilo ni ya kipekee, kutokana kujengwa likiwa ng’ambo ya pili, na baada ya kukamilika husukumwa hadi sehemu yake, kuunganisha kingo mbili, na kuwa tayari kwa ajili ya matumizi ya kivuko.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

February 19, 2026

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

February 14, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025347

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024233

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

By Mbeya YetuFebruary 19, 20265

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani…

Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ashiriki kampeni ya kitaifa ya uwekezaji wa ndani.

February 18, 2026

MBEYA YAANDIKA HISTORIA: NGazi ZA UMEME ZA KWANZA NYANDA ZA JUU KUSINI

February 18, 2026

ZIMAMOTO WAOPOA MWILI WA KIJANA ALIYEDAIWA KUWA MWANAFUNZI WA CBE MBEYA

February 17, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

February 19, 2026

Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ashiriki kampeni ya kitaifa ya uwekezaji wa ndani.

February 18, 2026

MBEYA YAANDIKA HISTORIA: NGazi ZA UMEME ZA KWANZA NYANDA ZA JUU KUSINI

February 18, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025347

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024233
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.