Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha CICG, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 24 Machi, 2024.
Mkutano huo unatarajiwa kujadili Dhima Kuu ambayo ni “Matumizi ya Diplomasia ya Kibunge katika kuleta Amani na Maelewano Duniani”. Mkutano huo umehudhuriwa na Maspika wa Mabunge 48 na washiriki zaidi ya 1,500 na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27 Machi, 2024.
Huu unakuwa Mkutano wake wa kwanza kuufungua tangu achaguliwe kuwa Rais wa IPU katika Uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, 2023 nchini Angola. 
Trending
- Serie A yampa fedha baada ya kubaini mbinu bora ya betting
- Hatua moja muhimu ya kufanikiwa kibiashara
- MSIGWA Atoa Onyo kwa Vyombo vya Habari vya Nje: Zingatia Maadili
- Namna ya kuimarisha ustawi wa ndoa yako
- RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA
- Rungwe Wasaini Mkataba wa Bilioni 2.8 Kujenga Soko la Kisasa la Ndizi
- Safari Kuelekea Furaha ya Ndoa Iliyokosekana Kwa Muda Mrefu
- Badili upepo wa Biashara Yako Hadi Mafanikio

