Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha CICG, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 24 Machi, 2024. Mkutano huo unatarajiwa kujadili Dhima Kuu ambayo ni “Matumizi ya Diplomasia ya Kibunge katika kuleta Amani na Maelewano Duniani”. Mkutano huo umehudhuriwa na Maspika wa Mabunge 48 na washiriki zaidi ya 1,500 na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27 Machi, 2024. Huu unakuwa Mkutano wake wa kwanza kuufungua tangu achaguliwe kuwa Rais wa IPU katika Uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, 2023 nchini Angola.
Trending
- MH. MAHUNDI VIJANA TUACHE KUTUMIA MITANDAO VIBAYA
- Bosi wangu anang’ang’ania kuzaa mtoto na mke wangu!
- ONYO:”WANACCM MBEYA WATAKAOWAINGILIA WABUNGE MAJIMBONI MWAO KABLA YA KAMPENI KUKIONA CHA MOTO”
- KADA WA CCM JIMBO LA RUNGWE AIBUKA AELEZA MAFANIKIO YA RAIS SAMIA NA MBUNGE MWANTONA JIMBONI
- Njia ya kuwafanya watoto wako wafaulu mitihani yao hadi Chuo Kikuu
- Agizo la RC.Homera Kwa TARURA na Mkandarasi Laanza Kutekelezwa Ndani ya Siku Moja kifusi chasambazwa
- Baada ya kufunga harusi ya Sh200 milioni, nimemfumania mke wangu na house boy!
- RC. Homera atoa siku saba kwa mkandarasi kufikisha vifaa katika eneo la mradi wa barabara Iziwa