Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilikuwa Mwembamba Kupita Kiasi Licha ya Kula Vizuri Hatua Nilizochukua Kuanza Kuongeza Uzito kwa Afya

January 4, 2026

Nilikuwa Nakunjamana kwa Maumivu Kila Nikifika Siku Zangu Njia Nilizojifunza Kudhibiti Maumivu ya Hedhi Bila Kukata Tamaa

January 4, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATOA TABASAMU KWA KITUO CHA TUMAINI LA WAZEE JIJINI MBEYA.

January 4, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilikuwa Mwembamba Kupita Kiasi Licha ya Kula Vizuri Hatua Nilizochukua Kuanza Kuongeza Uzito kwa Afya
  • Nilikuwa Nakunjamana kwa Maumivu Kila Nikifika Siku Zangu Njia Nilizojifunza Kudhibiti Maumivu ya Hedhi Bila Kukata Tamaa
  • NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATOA TABASAMU KWA KITUO CHA TUMAINI LA WAZEE JIJINI MBEYA.
  • LIVE: JUBILEE YA MIAKA 25 KATIKA NDOA. YA MR. & MRS. PATRICK ADKIN MWALUNENGE
  • Alinilikataa Kimapenzi Mara Kadhaa Hatua Moja Iliyobadilisha Mtazamo Wake
  • Hatua Moja Iliyanifanya Nimepata Mali Yangu
  • Mtoto Wangu Alichelewa Kutembea na Kuongea Hatua Moja Iliibua Maendeleo Yake
  • Nilianza Januari Bila Pesa ya Mahitaji Hatua Moja Ilinisaidia Kusimama Tena
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home ยป MIAKA MITATU YA SAMIA TANRODS MBEYA YAONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI
Habari za Kitaifa

MIAKA MITATU YA SAMIA TANRODS MBEYA YAONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMarch 26, 2024No Comments31 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini(TANRODS)Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari amesema miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa Mkoani Mbeya katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani.Masige ameyasema hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya huku akiitaja mitandao mbalimbali ya barabara za TANROADS ambazo inatekelezwa ni kuwa jumla ya kilometa 1,403.3 ambapo kati ya hizo kilometa 469.3 ni barabara za lami na kilometa 934 ni za changarawe. Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara za lami kuwa ni pamoja mradi wa njia nne kuanzia Nsalaga-lfisi kilometa 29 unaogharimu shilingi bilioni 138.718.Barabara nyingine ni ya Ibanda-Kajunjumele-Kiwira na Itungi Port kilometa 32 unaogharimu shilingi bilioni 38.359,mradi mwingine ni Katumba-Mbambo-Tukuyu Bujesi -Mbambo kilometa 10 na Tukuyu-Mbambo kilometa 7 kwa gharama ya shilingi bilioni 21.307.Aidha Masige amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Dkt Samia Suluhu Hassan serikali imejenga kituo cha huduma ya pamoja mpakani Kasumulu(Tanzania/Malawi)kwa gharama ya ya shilingi bilioni 26.4 mrdi huo umefikia asilimia zaidi ya 90 na sasa uepunguza msongamano wa magari,mradi mwingine umehusisha ukarabati wa uwanja wa ndege jengo la abiria pia njia ya kuruka na kutua ndege sanjari na kuweka taa za kuongoza ndege kwa gharama ya shilingi bilioni 33.8 ambapo kwa sasa uwanja unafanya kazi kwa saa 24 hivyo umeongeza pato la serikali. Hata hivyo Mhandisi Masige Matari amesema serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya lami lgawa-Tunduma kilometa 218 pamoja na Uyole-Songwe batabara ya mchepuko kilometa 48.9 ambapo ikikamilika mbali ya kupunguza msongamano itasaidia kupunguza ajali.

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini(TANRODS)Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari amesema miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa Mkoani Mbeya katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani.

Masige ameyasema hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya huku akiitaja mitandao mbalimbali ya barabara za TANROADS ambazo inatekelezwa ni kuwa jumla ya kilometa 1,403.3 ambapo kati ya hizo kilometa 469.3 ni barabara za lami na kilometa 934 ni za changarawe.

Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara za lami kuwa ni pamoja mradi wa njia nne kuanzia Nsalaga-lfisi kilometa 29 unaogharimu shilingi bilioni 138.718.

Barabara nyingine ni ya Ibanda-Kajunjumele-Kiwira na Itungi Port kilometa 32 unaogharimu shilingi bilioni 38.359,mradi mwingine ni Katumba-Mbambo-Tukuyu Bujesi -Mbambo kilometa 10 na Tukuyu-Mbambo kilometa 7 kwa gharama ya shilingi bilioni 21.307.

Aidha Masige amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Dkt Samia Suluhu Hassan serikali imejenga kituo cha huduma ya pamoja mpakani Kasumulu(Tanzania/Malawi)kwa gharama ya ya shilingi bilioni 26.4 mrdi huo umefikia asilimia zaidi ya 90 na sasa uepunguza msongamano wa magari,mradi mwingine umehusisha ukarabati wa uwanja wa ndege jengo la abiria pia njia ya kuruka na kutua ndege sanjari na kuweka taa za kuongoza ndege kwa gharama ya shilingi bilioni 33.8 ambapo kwa sasa uwanja unafanya kazi kwa saa 24 hivyo umeongeza pato la serikali.

Hata hivyo Mhandisi Masige Matari amesema serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya lami lgawa-Tunduma kilometa 218 pamoja na Uyole-Songwe batabara ya mchepuko kilometa 48.9 ambapo ikikamilika mbali ya kupunguza msongamano itasaidia kupunguza ajali.

Mradi mwingine unaotarajiwa kutekelezwa ni mradi wa Katumba-Mbambo-Tukuyu sehemu ya Katumba-Lupaso kilometa 35.3 Mbaka-Kibaji wenye urefu wa kilometa 20.7

Masige amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Mbeya jumla ya fedha zilizopokelewa hadi mwezi machi,2024 ni kama ifuatavyo:-
(i)Fedha za matengenezo shilingi bilioni 32.089

(ii)Fedha za miradi ya maendeleo shilingi bilioni 124.923.

Miradi iliyokamilika mpaka sasa ni pamoja na barabara ya Chunya -Makongolosi yenye urefu wa kilometa 39 pamoja na mzani wa Matundasi kwa gharama ya shilingi bilioni 67 ambapo barabara hi imeongeza thamani ya mazao na madini ya dhahabu katika Wilaya ya Chuya,barabara nyingine ni ya Kikusya-lpinda-Matema yenye urefu wa kilomet 39.1 kwa gharama ya shilingi bilioni 63.3 barabara hii imekuwa sehemu ya utalii wa fukwe za Ziwa Nyasa na safu za milima ya Livingstone.

Kukamilika kwa mtandao wa barabara Mkoani Mbeya mbali ya kuongeza pato la serikali utafungua fursa za utalii kutokana na wageni watakaotumia,Barabara ya TANZAM,Uwanja wa Ndege wa Songwe,Bandari ya Itungi na Mpaka wa Kasumulu.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATOA TABASAMU KWA KITUO CHA TUMAINI LA WAZEE JIJINI MBEYA.

January 4, 2026

MDAU WA MAENDELEO NDELE MWASELELA AYAJENGA NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA

January 1, 2026

WANANCHI HAI, FUONI , KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO

December 29, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025291

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025239

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024213

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025132
Don't Miss
Uncategorized

Nilikuwa Mwembamba Kupita Kiasi Licha ya Kula Vizuri Hatua Nilizochukua Kuanza Kuongeza Uzito kwa Afya

By Mbeya YetuJanuary 4, 20263

Kwa muda mrefu nilikuwa mtu wa kuonewa huruma. Nilikuwa nakula kama wengine, wakati mwingine hata…

Nilikuwa Nakunjamana kwa Maumivu Kila Nikifika Siku Zangu Njia Nilizojifunza Kudhibiti Maumivu ya Hedhi Bila Kukata Tamaa

January 4, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATOA TABASAMU KWA KITUO CHA TUMAINI LA WAZEE JIJINI MBEYA.

January 4, 2026

LIVE: JUBILEE YA MIAKA 25 KATIKA NDOA. YA MR. & MRS. PATRICK ADKIN MWALUNENGE

January 3, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilikuwa Mwembamba Kupita Kiasi Licha ya Kula Vizuri Hatua Nilizochukua Kuanza Kuongeza Uzito kwa Afya

January 4, 2026

Nilikuwa Nakunjamana kwa Maumivu Kila Nikifika Siku Zangu Njia Nilizojifunza Kudhibiti Maumivu ya Hedhi Bila Kukata Tamaa

January 4, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATOA TABASAMU KWA KITUO CHA TUMAINI LA WAZEE JIJINI MBEYA.

January 4, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025291

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025239

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024213
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.