Tarehe 27.11.2024 saa 12:30 jioni eneo la Mbembela Jijini Mbeya katika
barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, Gari lori namba T.537 DNC na Tela
namba T.241 ARG aina FAW iliyokuwa imepakia madini ya Sulphur ikitokea
Dar es Salaam kuelekea Tunduma Mkoa wa Songwe ilipoteza uelekeo na
kugonga magari sita, bajaji nne, Pikipiki moja na kusababisha vifo vya watu
watatu, wawili papo hapo na mmoja amefariki dunia leo Novemba 28, 2024
akiwa anaendelea na matibabu.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T.199 DYF Toyota Coaster, SU 44682
Toyota Double Cabin mali ya Shirika la Posta Mbeya iliyokuwa ikiendeshwa na
Fredy Mwasanga [48] mkazi wa Soweto, Gari T.134 DXK Toyota Double Cabin
iliyokuwa ikiendeshwa na Lusekelo Mwaseba [48] mkazi wa Sae, Gari T.370
ABN Toyota Land Cruiser, Gari T.344 BTS Toyota Cresta na Gari T.474
EHL/t.449 EHL aina ya FAW iliyokuwa ikiendeshwa na Alon Ruben [50] mkazi
wa Isanga.
Aidha, katika ajali hiyo Bajaji nne ziligongwa ambazo ni MC.446 DYK, MC.649
DWL, MC.138 DKC na MC.261 EBN na Pikipiki moja ambayo haijafahamika
namba zake za usajili. Waliofariki katika ajali hiyo bado hawajatambulika,
wawili jinsia ya kiume na mmoja jinsia ya kike. Majeruhi tisa wanaendelea na
matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kushindwa kulimudu Gari kwenye
eneo lenye mteremko. Jitihada za kumtafuta Dereva kwa kushirikiana na
mmiliki wa Gari zinaendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa madereva kuwa
makini na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza
kuepukika.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Trending
- MWALUNENGE AWAUNGANISHA VIJANA KIWIRA, WALA CHAKULA PAMOJA NA POLISI KUSHEREHEKEA KRISMASI KWA AMANI
- Shinikizo la Damu Liliendelea Kunisumbua Hatua Moja Ndogo Ilinirejesha Afya Yangu
- Jinsi Nilivyorejesha Heshima Yangu Baada Ya Mjomba Kunisaliti Ndoa Na Ukweli Kujitokeza Bila Vurugu
- Nilijaribu Kila Njia Kuokoa Uhusiano Wangu Ulioathirika na Pombe Hii Njia Ilifanya Kila Kitu Rahisi
- Ulinzi Mkali Waimarishwa Kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya 2026 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
- MSHTUKO MBEYA: MTOTO DARASA LA SABA AUAWA KWA KIPANDE CHA MTI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAYAI
- Nilipoteza Amani Bila Sababu Inayoonekana Ufafanuzi wa Kienyeji Ulinipa Mwanga
- MH. MAHUNDI AWAHIMIZA VIJANA KUISHI KWA MISINSI YA UWAJIBIKAJI NA UTU

