Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa taarifa ya kifo kilichohusisha
watu watano wa familia moja huko Wilaya ya Chunya.
Ni kwamba mnamo 29.12.2024 saa 8:30 usiku katika Kitongoji cha Nkangi
kilichopo Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe,
Wilaya ya Chunya, watu watano wa familia moja ya Masiganya Scania [39]
mfugaji, mkazi wa Nkangi walifariki dunia baada ya kupigwa radi kwenye
kambi ya kuchungia Ng'ombe wakati wakiwa wamelala.
Waliofariki katika tukio hilo ni Balaa Scania [28], Kulwa Luweja [17], Masele
Masaganya [16], Hema Tati [10] na Manangu Ngwisu [18] wote wakazi wa
Kijiji cha Nkangi. Aidha, katika tukio hilo watu wengine watano walijeruhiwa
ambao ni Gulu Scania [30], Manyenge Masaganya [13], Seni Solo [13],
Paskali Kalezi [16] na Huzuni Kalezi [19] wote wakazi wa Kijiji cha Nkangi.
Chanzo cha tukio hilo ni mvua kubwa iliyonyesha usiku ikiambatana na radi
hivyo kusababisha vifo vya watu watano na wengine watano kujeruhiwa.
Majeruhi walikimbizwa katika Kituo cha Afya Isangawana kwa matibabu na
walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali zao kuwa nzuri.
Trending
- Baada ya hapo ndipo akapata kazi kubwa zaidi!
- SIMBACHAWENE ATEMBEA MITAANI KUANGALIA USALAMA—AWAPA HONGERA WANANCHI KWA UTULIVU
- Taarifa nyingine Tena Toka jeshi la polisi
- 2021 11 26 14 36 44
- SHILINGI BILIONI 6.7 KUTIBU WAGONJWA 760 WASIO NA UWEZO WA KUMUDU GHARAMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA
- Polepole hisia zilianza kurejea na maisha yalianza upya!
- Jeshi la Polisi latoa Taarifa muda huu
- Hali shwari Jiji la Mbeya

