Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa taarifa ya kifo kilichohusisha
watu watano wa familia moja huko Wilaya ya Chunya.
Ni kwamba mnamo 29.12.2024 saa 8:30 usiku katika Kitongoji cha Nkangi
kilichopo Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe,
Wilaya ya Chunya, watu watano wa familia moja ya Masiganya Scania [39]
mfugaji, mkazi wa Nkangi walifariki dunia baada ya kupigwa radi kwenye
kambi ya kuchungia Ng'ombe wakati wakiwa wamelala.
Waliofariki katika tukio hilo ni Balaa Scania [28], Kulwa Luweja [17], Masele
Masaganya [16], Hema Tati [10] na Manangu Ngwisu [18] wote wakazi wa
Kijiji cha Nkangi. Aidha, katika tukio hilo watu wengine watano walijeruhiwa
ambao ni Gulu Scania [30], Manyenge Masaganya [13], Seni Solo [13],
Paskali Kalezi [16] na Huzuni Kalezi [19] wote wakazi wa Kijiji cha Nkangi.
Chanzo cha tukio hilo ni mvua kubwa iliyonyesha usiku ikiambatana na radi
hivyo kusababisha vifo vya watu watano na wengine watano kujeruhiwa.
Majeruhi walikimbizwa katika Kituo cha Afya Isangawana kwa matibabu na
walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali zao kuwa nzuri.
Trending
- Baada ya kuijua Nyota yangu ndipo nikafanikiwa haraka maishani
- SIKU NMB MASTABATA ILIVYOWAPIGISHA SHOPPING YA KIBABE WATEJA WAKE MBEYA
- Naibu Waziri Mahundi Aongoza Sherehe ya WAWATA, Mbeya
- RC. Homera: Endeleeni kukiamini chama Cha Mapinduzi kitawaletea Mambo mengi
- “RC Homera: Tuwatafute Popote Walipo Watu Wenye Ulemavu, Tuwape Mikopo”
- MAHUNDI ACHANGIA 2M KIKUNDI CHA IVIMA MAKONGOROSI CHUNYA
- Naota nanyongwa na rafiki zangu, nikiamka nimewasahau!
- WAKAZI MTAA WA KATI SOWETO MBEYA WAINGIA MTAANI WAJITENGENEZEA BARABARA ILIYOHARIBIWA NA MVUA