Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson ametoa Msaada wa Kumsomesha Yohana Japhet anayeishi Kwenye Mazingira Magumu.
Yohana anayeishi na Bibi yake Mlezi Katika Kata ya Ilomba Mtaa wa Ituha Mbeya Mjini anasoma Darasa la Saba hapo awali alikuwa akifanya Kazi ya Kuponda Kokoto Ili apate Fedha Kwaajili ya kununua Mahitaji Mbalimbali ya Shule na Chakula.
Mhe. Dkt. Tulia Ackson amemtembelea Kijana huyo na Kuahidi Kumsomesha hadi atakapofikia ukomo wa Masomo yake pia amemsaidia Bibi yake Chakula (Mchele Kilo 40) na Mavazi (Nguo na Blanket).