CHUNYA YAFIKIWA NA MKONGA WA TAIFA WA MAWASILIANO
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea Kituo cha mkonga wa Taifa cha mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kilichojengwa kwa lengo la kuboresha mawasiliano na ili kuongeza ufanisi kwa watendaji wa serikali katika makusanyo ya Serikali.
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya mawasilano kupitia ujenzi wa vituo mkongo wa taifa nchikavu na baharini, ambapo amesema kupitia uwekezaji huo Wilaya 139 nchini zitanufaika na huduma ya mkongo wa Taifa hivyo kurahisisha utendaji wa Serikali.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya na Songwe Mhandisi Mujuni Kyaruzi amesema mkongo huo utaunganisha mkoa wa Mbeya na mkoa wa Songwe kupitia Wilaya ya Songwe ambapo unatarajiwa kuanza kutumika mwezi Aprili mwaka huu baada ya kukamilika ufungaji wa waya eneo la kilomota 10 lililobaki.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Alhaj Batenga amesema wananchi wachangamkie fursa hiyo ya ujiio wa mkongo wa Taifa kwani kwa sasa kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali kutokana na changamoto ya mawasiliano maeneo mengi ya Wilaya hiyo, huku akiwataka wananchi kuilinda miundombinu hiyo ili Taifa liendelee kukua kiuchumi.