Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA NA MAELEKEZO YA KUPIGA KURA MAJIMBO YA MBEYA MJINI NA UYOLE

October 21, 2025

Maelfu ya wana CCM Mbeya Wamiminika Songwe Kumlaki Dkt. Samia—Wavutiwa na Uongozi Wake wa Kipekee

October 20, 2025

Nilivamiwa na Uchawi Kila Usiku Hadi Nilipopata Kinga Iliyowafanya Wachawi Washindwe Kunitazama Machoni

October 19, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA NA MAELEKEZO YA KUPIGA KURA MAJIMBO YA MBEYA MJINI NA UYOLE
  • Maelfu ya wana CCM Mbeya Wamiminika Songwe Kumlaki Dkt. Samia—Wavutiwa na Uongozi Wake wa Kipekee
  • Nilivamiwa na Uchawi Kila Usiku Hadi Nilipopata Kinga Iliyowafanya Wachawi Washindwe Kunitazama Machoni
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAKASUNGWA JIMBO LA BUCHOSA
  • RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania
  • Nilivyolipizwa Kisasi na Aliyeniumiza Baada ya Kunitendea Vibaya, Sasa Anaomba Msamaha Kila Siku
  • Nilivyomrudisha Mume Wangu Baada ya Miaka Mitatu ya Kuachana, Sasa Hachoki Kuniambia ‘You’re My Destiny
  • Madaktari Walishangaa Nilivyopona Maradhi Ambayo Walikuwa Wamesema Hayatibiki
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA YAFUNGULIWA LEO
Habari za Kitaifa

MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA YAFUNGULIWA LEO

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJanuary 18, 2025Updated:January 18, 2025No Comments4 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mwenyekiti wa tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele akifungua mafunzo ya siku
mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa
Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na
Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 17 hadi 18 Januari, 2025
Mkoani Mtwara ambapo amewataka watendaji hao kuhakikisha wanatunza vifaa vya
uandikishaji ili viweze kutumika katika maeneo mengine nchini pamoja na kuzangitia
mafunzo hayo ili wakafanikishe zoezi hilo muhimu.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani humo linataraji kuanza Januari 28,2025 na kufikia tamati Februari 03,2025 huku vituo vikitaraji kufunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:jioni kwa siku zote saba.

 

 

 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi, Ndg. Kailima, R. K akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa
wa Mtwara, Fredrick Mwanamboje akiwasilisha mada ya uraia kwa watendaji wa
uboreshaji mkoa wa Mtwara wakati wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji hao
ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani huo.
Watendaji hao ni pamoja na Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa
Waandikishaji, Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa
Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.

 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 17 Januari, 2025 amefungua mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Lindi ambapo amewataka watendaji hao kutunza vifaa vya uboreshaji wa Daftari na kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wote wa utendaji wao.

 

 

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huo ambao utafanyika sambamba na Mkoa wa Mtwara na mkoani Ruvuma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru kuanzia tarehe 28 Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari, 2025 na ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

 

 

 

Na
Waandishi wetu,

Mafunzo
kwa Watendaji wa uchaguzi katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma katika
halmashauri za wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru ikiwa ni mzunguko wa 10 wa
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yamefunguliwa leo mkoani Mtwara na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe.
Jacobs Mwambegele.


Mafunzo
kama hayo pia yamefunguliwa katika mikoa ya Lindi na Ruvuma ambapo mkoani Lindi
mafunzo hayo yamefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani (Mstaafu)
Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk na mkoani Ruvuma, mafunzo hayo yamefunguliwa na
Mjumbe wa Tume Mhe. Magdalena Rwebangira.

Akifungua
mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa
Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa
Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe
17 hadi 18 Januari, 2025 Mkoani Mtwara Mhe. Jaji Mwambegele amewataka watendaji
hao kuhakikisha wanatunza
vifaa vya uandikishaji ili viweze kutumika katika maeneo mengine nchini.

Amesema
ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji
wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa
gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya
uandikishaji nchini.

Mkoani
Lindi, Makamu Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu
Mbarouk Salim Mbarouk amewaambia watendaji hao kuwa  wakati wa uboreshaji wa Daftari  katika mikoa hiyo, mawakala wa vyama vya siasa
wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo
litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia
kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa
za lazima.

Amewaambia
watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa
wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo
litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia
kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa
za lazima.

Hata
hivyo Mhe. Jaji Mbarouk amesisitiza kuwa mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji
wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Naye
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Rwebangira ambaye
amefungua mafunzo hayo kwa watendaji wa uboreshaji katika mkoa wa Ruvuma ameeleza
kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea umahiri watendaji hao ili waweze
kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa
mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi
ambao ndio watakaohusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni.

Ameongeza
kuwa Maafisa TEHAMA nao watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati
wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.

Mafunzo
hayo ambayo yanafanyika kwa muda wa siku mbili ni sehemu ya maandalizi ya
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa ya Mtwara, Lindi na
Ruvuma katika halmashauri za wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru ambao
utafanyika kuanzia tarehe 28 Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari, 2025.

 

Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wamekula kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Mtwara, Mhe. Lucas Jang’andu ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji ngazi ya mkoa katika Mkoa wa Mtwara. 
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAKASUNGWA JIMBO LA BUCHOSA

October 18, 2025

RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania

October 18, 2025

MAWAZIRI WAIMWAGIA PONGEZI BENKI YA NMB KWA UTENDAJI WAKE.

October 13, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024193

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025184

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025126
Don't Miss
Video Mpya

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA NA MAELEKEZO YA KUPIGA KURA MAJIMBO YA MBEYA MJINI NA UYOLE

By Mbeya YetuOctober 21, 20252

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.

✅ Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.
✅ Vituo vya magereza vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.
✅ Kila mpiga kura anatakiwa kufika kituoni na kadi yake ya kupigia kura.
✅ Waliopoteza kadi wataruhusiwa kutumia NIDA, leseni au pasi ya kusafiria endapo jina lipo kwenye daftari la wapiga kura.

🗓️ Taarifa hii imetolewa na Ms. Anamary Joseph Mbunga, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini – tarehe 19 Oktoba 2025.

Maelfu ya wana CCM Mbeya Wamiminika Songwe Kumlaki Dkt. Samia—Wavutiwa na Uongozi Wake wa Kipekee

October 20, 2025

Nilivamiwa na Uchawi Kila Usiku Hadi Nilipopata Kinga Iliyowafanya Wachawi Washindwe Kunitazama Machoni

October 19, 2025

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAKASUNGWA JIMBO LA BUCHOSA

October 18, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA NA MAELEKEZO YA KUPIGA KURA MAJIMBO YA MBEYA MJINI NA UYOLE

October 21, 2025

Maelfu ya wana CCM Mbeya Wamiminika Songwe Kumlaki Dkt. Samia—Wavutiwa na Uongozi Wake wa Kipekee

October 20, 2025

Nilivamiwa na Uchawi Kila Usiku Hadi Nilipopata Kinga Iliyowafanya Wachawi Washindwe Kunitazama Machoni

October 19, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024193

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025184
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.