Wananchi wa Kata ya Itewe, wilayani Chunya, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika ujenzi wa daraja jipya ambalo limeboresha miundombinu na kurahisisha usafiri katika eneo hilo. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Juma Zuberi Homera, amepongeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

