Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

February 11, 2026

CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.

February 11, 2026

DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji

February 10, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya
  • CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.
  • DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji
  • KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA
  • Wilaya ya Mbeya Yapiga Marufuku Kilimo na Ukataji Miti Kwenye Vyanzo vya Maji
  • Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo
  • TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya
  • New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WAANDISHI WA HABARI KUANZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAI-HABARI – MSIGWA
Habari za Kitaifa

WAANDISHI WA HABARI KUANZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAI-HABARI – MSIGWA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMay 3, 2025No Comments13 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu, JAB

Serikali imesema vitambulisho vya Uandishi wa Habari (Press Card), vitaanza kutolewa wakati wowote baada ya siku saba kuanzia leo Mei 3, 2025 baada ya Waandishi wa Habari kuanza kujisajili rasmi kwenye mfumo wa TAI-Habari.

Mwandishi wa Habari ataanza kujisajili kupitia kiunganishi cha https://taihabari.jab.go.tz kisha kufuata maelekezo yaliyotolewa ili kukamilisha kujaza fomu yake kwenye mfumo huo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.

Kauli hiyo imetolewa tarehe 03 Mei, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, katika Kijiji cha Sayu mkoani Shinyanga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali ya Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.

“Tuliwaahidi kwamba tunawaletea Press Card (Vitambulisho vya kidijitali), ninayofuraha kuwajulisha kwamba ‘press card’ hizi za kidijital mchakato umekamilika, ziko tayari kwa matumizi, siku saba kuanzia sasa mtaingia kwenye kiunganishi cha Bodi ya lthibati ya Waandishi wa Habari na utaomba kitambulisho…,” alisema Bw. Gerson Msigwa.

Alisema Mwandishi wa Habari akishajaza taarifa zake sahihi, Bodi itapokea maombi na kuyahakiki na kama yamekidhi vigezo kitambulisho kitachapishwa na kutumwa mahali alipo kupitia Klabu za Waandishi wa Habari katika maeneo yao.

“Ombi langu kwenu Waandishi wa Habari mtambue kitambulisho hiki ni mali ya Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Tanzania…, hivyo ukipewa wewe ndiye utakayewajibika kwa lolote litakalofanyika kwa utambulisho wa kitambulisho hiki, siyo kitambulisho umekiacha huko, mtu amekichukua kaenda kufanya utapeli tutambaini kwa sababu sasa tutakuwa tunaweza kufuatilia kwa kupitia mfumo, tukibaini tutakupata wewe,” alisema Bw. Msigwa na kuongeza;

“Ninachowaomba kitunzeni kama mboni ya jicho, huu ndiyo utambulisho wenu wa kazi, muwe nacho mfukoni, usikiache hovyo hovyo.”

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula, ili kurahisisha zoezi la kutuma na kupokea Press Card hizo, Waandishi wa Habari wanahimizwa kujisajili kwenye Klabu za Waandishi wa Habari zilizopo maeneo yao.

Wakili Kipangula alisema wakati wa kujisajili Waandishi wa Habari wanapaswa kuweka kwenye mfumo vyeti vilivyo halali na kwamba ikiwa Mwandishi ataweka cheti cha kughushi, Bodi ya Ithibati itachukua hatua kali za kisheria kwa sababu hilo ni kosa la jinai.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA

February 10, 2026

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya

January 31, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025339

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024228

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025139
Don't Miss
Video Mpya

RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

By Mbeya YetuFebruary 11, 20265

CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.

February 11, 2026

DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji

February 10, 2026

KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA

February 10, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

February 11, 2026

CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.

February 11, 2026

DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji

February 10, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025339

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024228
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.