Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025

MA-EMSII MBEYA WALIA NA UTITIRI WA TOZO NA KODI KATIKA KAZI ZAO,DC ITUNDA AAHIDI KUTAFUTIA SULUHU

August 28, 2025

Wazazi Wafichua Mbinu Walizotumia Kuwalinda Watoto Wao Dhidi ya Jicho Baya na Uovu

August 28, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI
  • MA-EMSII MBEYA WALIA NA UTITIRI WA TOZO NA KODI KATIKA KAZI ZAO,DC ITUNDA AAHIDI KUTAFUTIA SULUHU
  • Wazazi Wafichua Mbinu Walizotumia Kuwalinda Watoto Wao Dhidi ya Jicho Baya na Uovu
  • MH. MICHAEL MAKAO ALIVYOREJESHA FOMU YA UDIWANI KATA RUJEWA AAHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA
  • Mwanamke Afumaniwa Akipika Chakula Usiku kwa Mtu Asiyeonekana, Jirani Atoa Neno
  • HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BAHATI NDINGO ALIPOKUWA AKIREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBARALI
  • Mwanamke miaka 50 aoana na kijana wa miaka 21 baada ya penzi lao kuvutia kijiji kizima kwa mshangao
  • KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home ยป Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Habari za Kitaifa

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 10, 2025No Comments23 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu

Serikali imekubali kutoa mafunzo maalum kwa waandishi wa blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, hatua muhimu itakayowajengea uwezo na kuwaandaa kubeba dhamana kubwa ya usambazaji wa habari sahihi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika Mkutamo wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya habari Katika kufanikisha uchaguzi Mkuu 2025.

Katika mkutano huo kipindi cha majadiliano Mwenyekiti wa Chama cha Mabloga Tanzania (TBN), Beda Msimbe, aliomba serikali kuona umuhimu wa kufunza mabloga wengi ambao sio waandishi lakini wanatengeneza maudhui kuwa na weledi kuandika masuala ya siasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Julai 9, 2025, Bwana Msimbe alisisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo mabloga, akibainisha kuwa, “Wao wanabeba dhamana kubwa kutokana na wingi wao na wanatengeneza maudhui, na wengine si waandishi wa habari.”

Aliongeza kuwa katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia na akili bandia (AI), vyanzo vya habari vinavyotegemewa zaidi si mitandao ya kijamii, bali maandishi yanayopatikana kwenye blogu na tovuti, hivyo kufanya uhitaji wa mafunzo kuwa mkubwa zaidi.

Bwana Msimbe alitumia fursa hiyo kupongeza uamuzi wa kuandaa kikao hicho muhimu cha wadau, akisema kuwa ni hatua inayostahili kuelekea uchaguzi wa haki na uwazi. Licha ya changamoto ya mada nyingi (tisa) kujadiliwa ndani ya siku moja, alipongeza mkutano huo na jinsi ulivyokwenda.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Ndugu Msigwa, aliiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuandaa mafunzo hayo mapema iwezekanavyo.

Kauli hiyo ya serikali imetafsiriwa na wadau mbalimbali kama hatua ya kutambuliwa rasmi kwa mchango wa mabloga katika tasnia ya habari na katika mchakato wa kidemokrasia.

Chama cha Mabloga Tanzania (TBN) kina wanachama zaidi ya 200 waliotawanyika kote nchini na nchi za nje, hivyo mafunzo haya yatakuwa na athari kubwa katika kuhakikisha usambazaji wa habari sahihi, zenye vigezo vya kitaaluma, na zinazozingatia maadili ya uandishi wa habari wakati wa kipindi cha uchaguzi na baadae.

Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko ambaye alitaka vyombo vya habari na vya usalama kuhakikisha Amani na kuvumiliana kuelekea katika uchaguzi huo.

mwisho

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Mbeya Yatikisika! Dkt. Tulia Achukua Fomu Ubunge Jimbo Jipya la Uyole

August 25, 2025

TAKUKURU Mbeya Yaokoa Milioni 47 na Kuongeza Mapato ya Halmashauri Zaidi ya Milioni 200

August 19, 2025

MGOMBEA NCCR MAGEUZI AJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA UTEUZI

August 15, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025204

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024183

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 202592

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202486
Don't Miss
Afya na Ustawi

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

By Mbeya YetuAugust 28, 202577

Imeelezwa kuwa uuguzi na ukunga ni fani ya wito wa kipekee na inayohitaji si maarifa…

MA-EMSII MBEYA WALIA NA UTITIRI WA TOZO NA KODI KATIKA KAZI ZAO,DC ITUNDA AAHIDI KUTAFUTIA SULUHU

August 28, 2025

Wazazi Wafichua Mbinu Walizotumia Kuwalinda Watoto Wao Dhidi ya Jicho Baya na Uovu

August 28, 2025

MH. MICHAEL MAKAO ALIVYOREJESHA FOMU YA UDIWANI KATA RUJEWA AAHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA

August 28, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025

MA-EMSII MBEYA WALIA NA UTITIRI WA TOZO NA KODI KATIKA KAZI ZAO,DC ITUNDA AAHIDI KUTAFUTIA SULUHU

August 28, 2025

Wazazi Wafichua Mbinu Walizotumia Kuwalinda Watoto Wao Dhidi ya Jicho Baya na Uovu

August 28, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025204

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024183

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 202592
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.