Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

DED MCHAU ATOBOA SIRI YA MAFANIKIO UFAULU KIDATO CHA SITA HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE

July 16, 2025

ANAYEFANYA KAZI BILA ‘PRESS CARD’ ANAVUNJA SHERIA

July 16, 2025

Dkt. Mpango: Ni Wakati wa Wanahabari Waafrika Kuandika Habari Chanya Kuhusu Afrika

July 16, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • DED MCHAU ATOBOA SIRI YA MAFANIKIO UFAULU KIDATO CHA SITA HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE
  • ANAYEFANYA KAZI BILA ‘PRESS CARD’ ANAVUNJA SHERIA
  • Dkt. Mpango: Ni Wakati wa Wanahabari Waafrika Kuandika Habari Chanya Kuhusu Afrika
  • WATENDAJI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 WAFUNDWA
  • WALIMU 900 SEKONDARI MIKOA SABA WAPEWA DOZI KUFUNDISHA TEHAMA, RC MALISA AFUNGUA MAFUNZO SIKU TANO
  • SIRI YA UTAJIRI WA MWALUNENGE HII HAPA AWEKA BAYANA HAJATUMIA UGANGA WA MIUJIZA
  • MSAADA WA DKT. TULIA WAFUTA MACHOZI YA FAMILIA YA BI. LUSIA KAPANGALA
  • BONANZA LA NMB MWALIMU SPESHO MBEYA VIBE LAKE LACHANGAMSHA WALIMU JIJINI MBEYA
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATENDAJI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 WAFUNDWA
Habari za Kitaifa

WATENDAJI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 WAFUNDWA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 16, 2025Updated:July 16, 2025No Comments1 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Julai 15,2025  amefungua  mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu  Mkoani Morogoro.
 
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa siku tatu na yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo.
 
Tume imeyagawa mafunzo hayo kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya kwanza inahusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndg. Kailima Ramadhani akizungumza jambo na washariki.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza  wakati wa  ufunguzi wa mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi Mkuu yaliyoanza leo Julai 15,2025 Mkoani Morogoro na kuwahusisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa,  Maafisa Uchaguzi, Maafisa Uchaguzi wasaidizi ngazi ya Jimbo kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida. (Picha na INEC).

 

Sehemu ya washiriki wa Mafunzo hayo.

 

 

Na. Mwandishi wetu.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa watendaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kufanya kazi kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume.
 
Hayo yamesemwa mkoani Morogoro leo Julai 15, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu kwa tarehe itakayotangazwa na Tume. 
 
Jitahidini na mjiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi. Hakikisheni mnazingatia ipasavyo Katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume, amesema Jaji Mwambegele.
 
Amewataka watendaji hao kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, sheria, kanuni na maelekezo ya Tume.
 
Amewasisitiza pia juu ya umuhimu wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi kwenye maeneo wanayopaswa kushirikishwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na maelekezo ya Tume.
 
Amewakumbusha kuhusu wajibu wao wa kuhakikisha wanavitambua vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husika na kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.
 
“Ajira za watendaji wa vituo zizingatie kuajiri watendaji wenye weledi, wanaojitambua, wazalendo, waadilifu na wachapakazi na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi, amesema Jaji Mwambegele. 

 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akifungua mafunzo hayo Unguja leo na amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka Tume, wanavihakiki, kuvikagua na kuhakikisha vinasambazwa kwenye vituo vyote na kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema

 

Washiriki kutoka Kisiwa cha Unguja mjini Zanzibar wakila kiapo cha kutunza siri na kujitoa uanchama.

 

 

Akifungua mafunzo kama hayo Mjini Unguja, Zanzibar, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka Tume, wanavihakiki, kuvikagua na kuhakikisha vinasambazwa kwenye vituo vyote na kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema.

 
“Wakati wa kuapisha mawakala, toeni taarifa mapema kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya Tume na kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala, amesema Jaji Mbarouk.
 
Amewataka kuhakikisha kuwa siku ya uchaguzi wanaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 kamili asubuhi na kufanya mawasiliano na Tume pale ambapo ushauri utahitajika kuhusiana na masuala ya uchaguzi.
 
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa siku tatu na yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo.
 
Tume imeyagawa mafunzo hayo kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya kwanza inahusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

ANAYEFANYA KAZI BILA ‘PRESS CARD’ ANAVUNJA SHERIA

July 16, 2025

Dkt. Mpango: Ni Wakati wa Wanahabari Waafrika Kuandika Habari Chanya Kuhusu Afrika

July 16, 2025

MSAADA WA DKT. TULIA WAFUTA MACHOZI YA FAMILIA YA BI. LUSIA KAPANGALA

July 13, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024174

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202484

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202460
Don't Miss
Video Mpya

DED MCHAU ATOBOA SIRI YA MAFANIKIO UFAULU KIDATO CHA SITA HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE

By Mbeya YetuJuly 16, 20250

#mbeyayetutv

ANAYEFANYA KAZI BILA ‘PRESS CARD’ ANAVUNJA SHERIA

July 16, 2025

Dkt. Mpango: Ni Wakati wa Wanahabari Waafrika Kuandika Habari Chanya Kuhusu Afrika

July 16, 2025

WATENDAJI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 WAFUNDWA

July 16, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

DED MCHAU ATOBOA SIRI YA MAFANIKIO UFAULU KIDATO CHA SITA HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE

July 16, 2025

ANAYEFANYA KAZI BILA ‘PRESS CARD’ ANAVUNJA SHERIA

July 16, 2025

Dkt. Mpango: Ni Wakati wa Wanahabari Waafrika Kuandika Habari Chanya Kuhusu Afrika

July 16, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024174

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202484

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.