Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Niliibiwa Gari Yangu Usiku, Lakini Hatua Niliyopiga Ilifanya Wezi Wenyewe Walirudishe Hadi Getini

September 16, 2025

Nilipoteza Mume Wangu Kwa Mpango wa Kando ila Kitu Nilichojaribu Kilimfanya Aombe Radhi Hadharani

September 16, 2025

Wezi walioiba gari langu waja nyumbani kujisalimisha wenye na kukiri makosa

September 16, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Niliibiwa Gari Yangu Usiku, Lakini Hatua Niliyopiga Ilifanya Wezi Wenyewe Walirudishe Hadi Getini
  • Nilipoteza Mume Wangu Kwa Mpango wa Kando ila Kitu Nilichojaribu Kilimfanya Aombe Radhi Hadharani
  • Wezi walioiba gari langu waja nyumbani kujisalimisha wenye na kukiri makosa
  • Shuleni walimuita “kichwa maji” ila sasa ana shule yake
  • Alipambana sana kupata mapenzi ya huyu binti bila mafanikio ila leo hii wapo pamoja
  • BRANDY NELSON:’NILIUKOSA UDIWANI V/MAALUM 2020 NIKAANZA UPYA 2025 CHAMA KIMENICHAGUA KUGOMBEA KATA’
  • Mwalunenge Aunguruma Kata ya Iganzo: Asema Oktoba Ni Kazi Moja tu – Rais, Mbunge na Madiwani CCM
  • HATIMAYEEE MGOMBEA UBUNGE CHAUMMA JIMBO LA UYOLE MBEYA AFUNGUKA
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
Habari za Kitaifa

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 18, 2025Updated:July 18, 2025No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Cyprian Mbugano, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa Uchaguzi kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida. 

 

 

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

 

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa ,Wasimamizi wa Uchaguzi,Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maofisa uchaguzi na maofisa ununuzi kutenga sehemu ya muda wao kusoma Katiba, sheria na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo.
 

 

Lengo  la kusoma Katiba,sheria na maelekezo mbalimbali  yanayotolewa na Tume hiyo  ili yawaongoze katika kusimamia vyema uchaguzi utakaokuwa huru na haki.
 

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Cyprian Mbugano, alisema hayo  jana kwa niaba ya  Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufaa, Jacobs wakati wa ufungaji  wa mafunzo  ya siku tatu kwa wasimamizi hao wapatao 165 kutoka halamshauri 24 za mikoa ya Dodoma , Singida na Morogoro.
 

 

Katika mafunzo hayo mada 12 ziliwasilishwa kwa washiriki kujifunza , na  kauli mbiu ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 ni ‘ Kura yako, Haki yako, Jitokeze kupiga kura”.
 

 

“ Kama ilivyoelezwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya , shughuli zote za uchaguzi zinaongozwa na Katiba , sheria , kanuni , maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume hivyo mkikutana na changamoto zozote msisite kufanya mawasilino na watendaji wa Tume ” alisema Mbugano .
 

 

“ Jukumu lililo mbele yenu ni kubwa na muhimu, linaahitaji umakini na kujitoa , hivyo ni matarajio ya Tume kwamba , baada ya kupatiwa mafunzo haya , mtatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na weledi mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka 2025 unaotarajiwa” alisisitiza Mbugano.
 

 

Kwa upande wa ajira za kupata watendaji wa vituo, alisema kuwa Tume inayoimani ya kwamba watateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo muhimu  , jambo ambalo limekuwa likisisitizwa tangu mwanzo wa mafunzo hayo.
 

 

“ Watendaji hawa wa vituo ndio watakaosimamia zoezi la kupinga kura na kuhesabu kura vituoni , kazi ambayo inahitaji umahiri , umakini na weledi katika kuitekeleza” alisisitiza Mbugano.
 

 

Alisema ni imani ya Tume kuwa mafunzo ya watendaji wa vituo yatafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi na yanalenga kuwajengea uwezo ili waweze kufahamu majukumu  yao na kuyatekeleza ipasavyo wakati wa uchaguzi.
 

 

Mbugano alitumia nafasi hiyo kuwaasa wasimamizi hao kubandika matangazo mbalimbali ya kisheria kuhusiana na uchaguzi pamoja na mabango mbalimbali yanayotakiwa kwa mujibu wa maelekezo .
 

 

Alisema ikumbukwe kuwa ,wapo wadau mbalimbali wa uchaguzi kama vile waangalizi wa uchaguzi kutoka ndani na n je ya nchi ambao wanafuatilia uendeshwaji wa uchaguzi na kiwango cha kuzingatiwaji wa sheria zinazohusiana na uchaguzi , hivyo wahakikishe wanazigatia  maelekezo yanayotolewa na Tume kila wakati.
 

 

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, Dismass Pesambili aliishukuru Serikali kupitia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwawezesha mafunzo hayo ambayo ni silaha na nyenzo muhimu ya kufanikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu .

 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MATIBABU YA KIBINGWA YA HUDUMA MKOBA YA MADAKTARI WA DT. SAMIA UKOMBOZI MKUBWA KWA WANANCHI WA MKOA WA SONGWE.

September 15, 2025

DKT. TULIA: NITAHAKIKISHA JIMBO JIPYA LA UYOLE LINAPATA HALMASHAURI

September 14, 2025

TUME YATOA MWALIKO KWA WAANDISHI WA HABARI WENYE NIA YA KURIPOTI MATUKIO WAKATI WA UCHAGUZI

September 3, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025208

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024184

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025125

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025124
Don't Miss
Uncategorized

Niliibiwa Gari Yangu Usiku, Lakini Hatua Niliyopiga Ilifanya Wezi Wenyewe Walirudishe Hadi Getini

By Mbeya YetuSeptember 16, 20250

Sikuwa na amani usiku ule nilipoamka ghafla saa tisa usiku nikakuta geti langu liko wazi.…

Nilipoteza Mume Wangu Kwa Mpango wa Kando ila Kitu Nilichojaribu Kilimfanya Aombe Radhi Hadharani

September 16, 2025

Wezi walioiba gari langu waja nyumbani kujisalimisha wenye na kukiri makosa

September 16, 2025

Shuleni walimuita “kichwa maji” ila sasa ana shule yake

September 16, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Niliibiwa Gari Yangu Usiku, Lakini Hatua Niliyopiga Ilifanya Wezi Wenyewe Walirudishe Hadi Getini

September 16, 2025

Nilipoteza Mume Wangu Kwa Mpango wa Kando ila Kitu Nilichojaribu Kilimfanya Aombe Radhi Hadharani

September 16, 2025

Wezi walioiba gari langu waja nyumbani kujisalimisha wenye na kukiri makosa

September 16, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025208

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024184

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025125
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.