Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Walisema kubashiri ni kupoteza muda, sasa mimi ndio nawakopesha pesa za kodi

August 1, 2025

MZRH YAWEKA HISTORIA KWA KUZINDUA CHUMBA CHA UPASUAJI KWA WATOTO

August 1, 2025

Mama mkwe alisema sitamzalia mwanae, leo ndio ananiletea zawadi kila wiki

August 1, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Walisema kubashiri ni kupoteza muda, sasa mimi ndio nawakopesha pesa za kodi
  • MZRH YAWEKA HISTORIA KWA KUZINDUA CHUMBA CHA UPASUAJI KWA WATOTO
  • Mama mkwe alisema sitamzalia mwanae, leo ndio ananiletea zawadi kila wiki
  • UTAINJOI VIJEMBE NA UTANI BAHATI NDINGO,MWAKABWANGA, MUBALI KAMPENI WATEULE WATANO JIMBO LA MBARALI
  • WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
  • Sikuwahi kuwaza kama nitakuja kuolewa katika umri huu
  • Nilikuwa naishi kwenye banda la mabati sasa majirani wanapiga picha kwenye nyumba yangu ya ghorofa
  • “MAHUNDI: Uongozi Wangu ni kwa Wanawake wa Mbeya – Asanteni kwa kuniamini tena
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
Habari za Kitaifa

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 31, 2025No Comments6 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 31,2025. 

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 31,2025. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg Kailima Ramadhani akitoa mada wakati wa Kikao cha Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 31,2025. 

 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg Kailima Ramadhani akitoa mada wakati wa Kikao cha Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 31,2025. 

 

 

 

Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mada.

 

Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
imeyataka makundi mbalimbali ya kijamii nchini kuyatumia majukwaa yao
kuwahamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wito huo umetolewa leo, tarehe 31 Julai
2025, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mheshimiwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mkutano kati ya Tume na
wawakilishi wa watu wenye ulemavu.

Katika hotuba yake, Jaji Mwambegele ameeleza
kuwa Tume inatambua na kuthamini mchango wa watu wenye ulemavu katika kueneza
taarifa sahihi na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi.

“Nawasihi kutumia majukwaa yenu kuhimiza
wenzenu kushiriki kwa amani na kuepuka kauli au vitendo vinavyoweza kuhatarisha
utulivu wa nchi yetu wakati wa kampeni,” amesema Mhe. Mwambegele, na kuongeza
kuwa Tume itaendelea kushirikiana nao katika hatua zote muhimu kuelekea
uchaguzi.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi
mkuu, Jaji Mwambegele amesema kuwa ratiba rasmi imeshatangazwa ambapo utoaji wa
fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi mbalimbali utafanyika kuanzia tarehe 9
Agosti hadi 27 Agosti 2025, huku kampeni zikipangwa kuanza tarehe 28 Agosti
hadi 28 Oktoba 2025 kwa upande wa Tanzania Bara.

Katika mkutano mwingine na wawakilishi
wa wanawake uliofanyika pia jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Tume,
Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufani (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, amewahimiza
wanawake kutumia nafasi zao kuwafikishia wananchi taarifa sahihi kuhusu hatua
za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, na kuhamasisha waliojiandikisha kwenye Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

Aidha, Jaji Mbarouk ametoa pongezi kwa
wanawake kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kipindi chote cha
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kilichoanza tarehe 20 Julai 2024
na kukamilika tarehe 4 Julai 2025.

“Natoa pongezi kwenu kwa namna
mlivyotuunga mkono wakati wote wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura. Tunawapongeza na tunawashukuru sana,” alisema Jaji Mbarouk.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Tume,
Mheshimiwa Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari, amewahimiza vijana kutumia
mitandao ya kijamii kwa uadilifu, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

“Natoa wito kwenu kuwahamasisha vijana
kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na kuepuka mitandao inayosambaza
habari za chuki na uchochezi,” amesema Jaji Asina.

Ameonya pia dhidi ya matumizi mabaya ya
teknolojia ya akiliunde (AI), ambayo kwa sasa inatumika kusambaza taarifa za
upotoshaji na chuki.

“Vilevile, muwakumbushe vijana wenzenu
kuepuka matumizi mabaya ya akiliunde. Vijana ni kundi lenye nguvu, na mkitambua
nafasi yenu, mtaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha uchaguzi
mkuu wa mwaka huu,” aliongeza.

Katika mikutano yote hiyo, viongozi wa
Tume wamekumbusha kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utafanyika kwa mujibu wa
sheria mbili mpya zilizopitishwa mwaka 2024, ambazo zimeleta maboresho ya
kiutendaji, kisheria na kiuwazi katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  uliowakutanisha Tume na wawakilishi wa wanawake kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025  jijini Dar es Salaam Julai 31, 2025.

 

 

Washiriki katika mkutano huo wa wakilishi wa wanawake wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. 

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Asina Omari akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  uliowakutanisha Tume na wawakilishi wa vijana kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam Julai 31, 2025.

 

Washiriki katika mkutano huo wa wakilishi wa Vijana wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. 

 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025

July 27, 2025

WATANZANIA MILIONI 37 KUPIGA KURA TAREHE 29 OKTOBA, 2025

July 26, 2025

Daraja la Masagi Wilayani Iramba kufungua mawasiliano vijijini

July 24, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024178

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 202599

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202581
Don't Miss
Uncategorized

Walisema kubashiri ni kupoteza muda, sasa mimi ndio nawakopesha pesa za kodi

By Mbeya YetuAugust 1, 20250

Moshi, Tanzania Wakati kijana mmoja mwenye umri wa miaka 29 akianza kucheza kamari mitandaoni miaka…

MZRH YAWEKA HISTORIA KWA KUZINDUA CHUMBA CHA UPASUAJI KWA WATOTO

August 1, 2025

Mama mkwe alisema sitamzalia mwanae, leo ndio ananiletea zawadi kila wiki

August 1, 2025

UTAINJOI VIJEMBE NA UTANI BAHATI NDINGO,MWAKABWANGA, MUBALI KAMPENI WATEULE WATANO JIMBO LA MBARALI

July 31, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Walisema kubashiri ni kupoteza muda, sasa mimi ndio nawakopesha pesa za kodi

August 1, 2025

MZRH YAWEKA HISTORIA KWA KUZINDUA CHUMBA CHA UPASUAJI KWA WATOTO

August 1, 2025

Mama mkwe alisema sitamzalia mwanae, leo ndio ananiletea zawadi kila wiki

August 1, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024178

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 202599

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.