Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Alishinda bahati nasibu ya kimataifa kwa tiketi ya mtandaoni na sasa anasafiri duniani kwa starehe

August 2, 2025

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

August 2, 2025

UZINDUZI WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA MWALIMU NYERERE

August 2, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Alishinda bahati nasibu ya kimataifa kwa tiketi ya mtandaoni na sasa anasafiri duniani kwa starehe
  • WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA
  • UZINDUZI WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA MWALIMU NYERERE
  • Nilivyopambana hadi kuishinda hali ya kuota ndoto za kutisha!
  • KAMPENI UBUNGE CCM MBEYA MJINI, NI MCHUANO MKALI KWA WAGOMBEA ZIMEBAKI SIKU MBILI
  • Walisema kubashiri ni kupoteza muda, sasa mimi ndio nawakopesha pesa za kodi
  • MZRH YAWEKA HISTORIA KWA KUZINDUA CHUMBA CHA UPASUAJI KWA WATOTO
  • Mama mkwe alisema sitamzalia mwanae, leo ndio ananiletea zawadi kila wiki
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA
Habari za Kitaifa

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 2, 2025No Comments9 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email


Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs
Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na Waandishi wa
Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja
kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 02 , 2025.

 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs
Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na Waandishi wa
Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja
kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 02 , 2025.

 

 

Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima
akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mkutano wa Tume na Waandishi wa
Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja
kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 02 , 2025. 
***************

 

Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kuhamasisha na kuelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba, 2025.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu, uliofanyika tarehe 2 Agosti, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Jaji Mwambegele amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu kwa kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi.
Ameeleza kuwa waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kutumia taaluma yao kuwaelimisha wananchi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ili waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amewakumbusha wanahabari wajibu wao wa kuhakikisha vyama vya siasa na wagombea wanapata nafasi ya kufikisha ujumbe wao kwa wapiga kura katika kipindi cha kampeni.
Aidha, Bw. Kailima amewataka wanahabari kutoa taarifa sahihi kwa umma na kuepuka kusambaza taarifa potofu katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na maadili ya taaluma ya habari.
Amewahimiza waandishi hao kutumia kalamu na nyenzo zao kueneza ujumbe wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ili kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha misingi ya demokrasia.
Pia amewaasa kuepuka kuchapisha au kurusha habari zinazoweza kuwavunja moyo wananchi na kuwafanya waone kama hakuna umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi, iwe ni kama wapiga kura au wagombea.
Mkutano kati ya Tume na Waandishi wa Habari ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya wadau mbalimbali ambayo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikiitisha katika maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mikutano hiyo ilianza tarehe 27 Julai 2025 kwa kukutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa, ikafuatiwa na mkutano na Wawakilishi wa Asasi Zisizo za Kiserikali kisha Wawakilishi wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari.
Mfululizo huu wa mikutano unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 4 Agosti 2025, baada ya mkutano na Waandaji wa Maudhui Mtandaoni, utakaofuatiwa na mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025

July 31, 2025

VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025

July 27, 2025

WATANZANIA MILIONI 37 KUPIGA KURA TAREHE 29 OKTOBA, 2025

July 26, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024178

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025119

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202581
Don't Miss
Uncategorized

Alishinda bahati nasibu ya kimataifa kwa tiketi ya mtandaoni na sasa anasafiri duniani kwa starehe

By Mbeya YetuAugust 2, 20251

Jina langu ni Saidi kutoka Tanga, na hadi leo bado siamini maisha niliyonayo sasa. Kuna…

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

August 2, 2025

UZINDUZI WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA MWALIMU NYERERE

August 2, 2025

Nilivyopambana hadi kuishinda hali ya kuota ndoto za kutisha!

August 2, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Alishinda bahati nasibu ya kimataifa kwa tiketi ya mtandaoni na sasa anasafiri duniani kwa starehe

August 2, 2025

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

August 2, 2025

UZINDUZI WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA MWALIMU NYERERE

August 2, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024178

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025119

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.