Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Dkt. Tulia Aongoza kwa Vitendo, Apiga Kura na Kuhamasisha Ushindi wa CCM Uyole

October 29, 2025

DKT MARY MWANJELWA AUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA AHAMASISHA KUJITOKEZA KWA WINGI AMANI IMETAWALA

October 29, 2025

Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu

October 27, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Dkt. Tulia Aongoza kwa Vitendo, Apiga Kura na Kuhamasisha Ushindi wa CCM Uyole
  • DKT MARY MWANJELWA AUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA AHAMASISHA KUJITOKEZA KWA WINGI AMANI IMETAWALA
  • Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu
  • MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”
  • “Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo
  • Nilivyomfanya Mtu Aliyenidharau Kuniheshimu na Kunitegemea Kwa Mambo Mengi
  • NABII MPANJI AUTANGAZIA UMMA, WAKRISTO WASISHIRIKI MAANDAMANO WAJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA
  • Nilivyookoa Biashara Yangu Baada ya Wateja Wote Kupotea Ghafla
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » Prof. Makulilo: Watanzania Wajiandae kwa Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050
Habari za Kitaifa

Prof. Makulilo: Watanzania Wajiandae kwa Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050

Mbeya YetuBy Mbeya YetuSeptember 17, 2025No Comments25 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mbeya – Mwenyekiti wa Kongamano na Mgoda wa Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu J.K. Nyerere katika Taaluma za Umajumui wa Afrika, Profesa Alexander Makulilo, amezungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya akitoa mwito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Prof. Makulilo alizungumza leo wakati akitoa taarifa rasmi kuhusu Kongamano la Uchumi Jumuishi kuelekea Dira 2050, ambalo limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu J.K. Nyerere kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre). Kongamano hilo limepangwa kufanyika tarehe 18 Septemba 2025, katika Ukumbi wa Nkrumah Lecture Theatre wa Chuo Kikuu Mzumbe – Ndaki ya Mbeya, kuanzia saa 5:00 asubuhi.

Umuhimu wa Kongamano

Akieleza sababu za kuandaliwa kwa kongamano hilo, Prof. Makulilo amesema uhitaji wake unatokana na mambo makubwa matatu. Kwanza, ni uzinduzi wa Dira 2050 uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Julai 2025 jijini Dodoma. Wakati huo, Rais alisisitiza juu ya kuimarishwa kwa mijadala ya kitaifa kuhusu maendeleo na nafasi ya vijana katika kuibeba Tanzania mpya.

“Mheshimiwa Rais alisisitiza kuwa ni lazima mijadala ya maendeleo irejee katika jamii yetu. Vijana ndio nguvu kazi ya taifa letu, na wao ndio wanapaswa kujipanga vyema ili kutimiza malengo ya Dira 2050,” alisema Prof. Makulilo.

Sababu ya pili ni maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, ambapo utekelezaji wa Dira 2050 utaanza rasmi. Kwa hiyo, kongamano litawajengea wananchi na wadau uwezo wa kutoa mapendekezo yatakayoingizwa kwenye utekelezaji wa mpango huo wa muda mrefu.

Sababu ya tatu ni maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2025/26 – 2029/30), ambao utajengwa kwa kuzingatia mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika mpango unaomalizika (2020/21 – 2025/26).

Mada Kuu

Kongamano hili litajadili mada nne kuu:

  1. Maudhui na Vipaumbele vya Dira 2050.

  2. Msingi wa Uchumi Jumuishi kuelekea Dira 2050, kwa kuangazia mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano unaomalizika.

  3. Nafasi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

  4. Uzoefu wa Sekta Binafsi kama kichocheo cha maendeleo endelevu na jumuishi.

Prof. Makulilo alisema kuwa mijadala hii inalenga kuleta uelewa wa pamoja, ushirikiano na mshikamano wa kitaifa katika utekelezaji wa dira hiyo kubwa ya maendeleo.

Washiriki Wakuu

Kongamano litashirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, sekta binafsi, asasi za kiraia, vyuo vikuu na washirika wa maendeleo. Baadhi ya watoa mada wakuu watakuwa:

  • Dkt. Fred Msemwa, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.

  • Ndugu David Kafulila, Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Centre.

  • Dkt. Gladness Salema, Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki.

  • Dkt. Mwajuma Hamza, Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania.

  • Prof. Humphrey Moshi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  • Dkt. Jasinta Kahyoza, Chuo Kikuu Mzumbe.

Mwito kwa Wananchi

Akihitimisha mkutano wake na waandishi wa habari, Prof. Makulilo ametoa mwito kwa wananchi na wadau wote kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo, ama kwa kufika Mbeya au kupitia vyombo vya habari.

“Kongamano hili ni la kitaifa. Tunawaalika wananchi wote na wadau kutoka sekta mbalimbali kushiriki nasi, kujifunza na kutoa maoni. Taarifa zitakuwa zikifikishwa mubashara kupitia ITV, na kupitia YouTube za Jambo TV na Global TV,” alisema.

Kwa mujibu wake, kongamano hili ni sehemu ya kuandaa taifa kuelekea safari ya kujenga Tanzania jumuishi, shirikishi na endelevu ifikapo mwaka 2050.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAKASUNGWA JIMBO LA BUCHOSA

October 18, 2025

RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania

October 18, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025202

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024196

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025126
Don't Miss
Video Mpya

Dkt. Tulia Aongoza kwa Vitendo, Apiga Kura na Kuhamasisha Ushindi wa CCM Uyole

By Mbeya YetuOctober 29, 20258

DKT MARY MWANJELWA AUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA AHAMASISHA KUJITOKEZA KWA WINGI AMANI IMETAWALA

October 29, 2025

Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu

October 27, 2025

MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”

October 27, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Dkt. Tulia Aongoza kwa Vitendo, Apiga Kura na Kuhamasisha Ushindi wa CCM Uyole

October 29, 2025

DKT MARY MWANJELWA AUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA AHAMASISHA KUJITOKEZA KWA WINGI AMANI IMETAWALA

October 29, 2025

Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu

October 27, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025202

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024196
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.