Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Tulia Ackson amesema kwenye Sekta ya kilimo ndani ya Kata ya Iganjo Mgombea Uraisi kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya Kazi Kubwa hasa Kuhakikisha Mbolea za Ruzuku na Pembejeo zote za kilimo hivyo ataendelea kuongeza upatikanaji maradufu wa Ruzuku na Pembejeo za kilimo.
Dkt. Tulia amesema anafahamu kwamba ndani ya kata hiyo Kuna kilimo cha umwagiliaji hivyo atahakikisha skimu zote za umwagiliaji zinabireshwa zadisi ili wakulima Wafanye kilimo Bora hivyo ifikapo 29 Oktoba 2025 Wananchi wakapige Kura nyingi kwa CCM ili wakulima wa Jimbo la Uyole wanufaike.
Akizungumza Katika Mkutano wa Kampeni zake Kata ya Iganjo eneo la Ilowe Sokoni ameendelea kuinadi Ilani ya CCM Kwa kuwaeleza Wananchi kuwa Sekta zote zitasimamiwa kikamilifu ili Wananchi waweze kupata Maendeleo ya Kweli hasa Sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu, Maji na uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Kampeni za Jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya “Uyole Kazi” ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.