Leo 1 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya CCM Dkt Tulia Ackson amesema ahadi zinazotolewa na Chama cha Mapinduzi kwa Wananchi ni zauhakika kwani zimekuwa zikitekelezeka kwa uhakika kutokana na Msimamizi Mzuri unaofanyika Chini ya Serikali inayoundwa na Chama hicho.
Akizungumza na Wananchi Kwenye Mkutano wake wa Kampeni eneo la Makondeko Sokoni Dkt. Tulia amesema mifano ya Jambo hilo ipo wazi, wakati anaomba ridhaa ya kuliongoza Jimbo la Mbeya Mjini aliahidi kupatikana kwa hospital ya Wilaya Jambo ambalo limekamika kwa kupata hospitali ya Igawilo ambayo inavifaa na Wataalamu wa kutosha, pia CCM iliahidi Ujenzi wa njia Nne kutoka Uyole – Ifisi Ujenzi huo unaendelea.
Katika hatua nyingine amewataka Wananchi wa Jimbo la Uyole na Watanzania kwa Ujumla Kukiamini Chama cha Mapinduzi na kuwapigua Kura nyingi Wagombea wa CCM 29 Oktoba 2025 ili wawaletee Maendeleo ya kweli kwani Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho imeeleza Mambo mazuri yenye kutekelezeka kwa manufaa ya Watanzania.
Sambamba na hayo amewaahidi Wakazi wa Kata ya Igawilo Kuboresha Miundombinu Kwenye Sekta ya Afya kwa Kuwajengea Zahanati, Kuendelea Kukarabati na Kujenga Madarasa Kwenye Shule zote, Kuwainua Wananchi Kiuchumi, Kuhakikisha wakulima wanapata Pembejeo za kilimo Kwa wakati, Kujenga Barabaraza Mitaa kwa Kiwango cha Lami pamoja na Kukarabati Reli ya Tazara Kama ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyosema.
Kampeni za Jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya “Uyole Kazi” ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.