Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Tulia Ackson amesema atahakikisha Wananchi wa Kata ya Mwakibete ambao hawajanufaika na Mradi wa REA wanafikiwa na Maradi huo ili kuondokana na Changamoto ya Kukosa Umeme.
Akizungumza Kwenye Mkutano wa Kampeni zake eneo la Magaerejini Mtaa wa Viwandani Kata ya Mwakibete amewaeleza Wananchi hao kuwa asilimia kubwa ya Wananchi wa Jimbo la Uyole wamefikiwa na Umeme wa REA hivyo atajitahidi kufuatilia ili huduma hiyo iweze kuwafikia wakazi Wote huku akiutaja maradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kama suluhisho la Kudumu kukatika kwa Umeme.
 
 
Katika hatua nyingine amewahakikishia Wananchi kunufaika na Mikopo ya Halmashauri ambayo kwenye ilani ya CCM imetajwa kuongezeka zaidi pia amesema ataendelea Kuhakikisha Miundombinu ya Elimu na Afya inaboreshwa zaidi ili Wakazi wa Kata hiyo wapate huduma Bora.
 
Sambamba na hayo Dkt. Tulia amesema Changamoto ya eneo la Kufanyia kazi Kwa Mafundi Geriji amelipatia ufumbuzi baada ya Mkurugenzi wa Jiji Kutoa eneo la Nane Nane Nane, Mlima nyoka na Igango hivyo amewataka mafundi hayo Kusubiri Maelekezo ya Mkurugenzi atakayoyatoa hivi karibuni Kuhusu Namna ya Kutumia Maeneo hayo.
 
Mwisho amewataka wakazi wa Mwakibete kuwachagua viongozi wa CCM kwa nafasi ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge Dkt. Tulia Ackson na Madiwani wa Chama hicho 29 Oktoba 2025 ili kwapamoja waweze kusukuma Maendeleo.
Kampeni za Jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya “Uyole Kazi” ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.
 

									 
					