Leo 04 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Tulia Ackson amesema kipaumbele kikubwa kwa sasa kwenye Sekta ya Afya Kata ya Mwansenkwa ni Kujenga Jengo la Mama na Mtoto pamoja na ukarabati wa Miundombinu kwenye Zahanati ya Kata hiyo.
Akizungumza Mbele ya wakazi wa Mwansenkwa kwenye Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika Mtaa wa Luala Dkt. Tulia amesema akipata ridhaa ya kuwaongoza Wananchi wa Jimbo la Uyole atahakikisha Jengo hilo linajengwa ili huduma ya Mama na Mtoto ipatikane jirani tofauti na ilivyo sasa.
Sambamba na hayo amesema ataendelea na zoezi la kutoa Bima za Afya kwa Wananchi wanaoishi kwenye Mazingira Magumu huku akisisitiza Changamoto ya uchakavu wa paa la Zahanati hiyo itamalizika kwani ameahidi kufanyia kazi kwa haraka zaidi kabla Mvua hazijaanza kunyesha.
 
 
 
Katika hatua nyingine Dkt. Tulia amewaeleza wananchi Mambo atakayoyafanya ikiwa ni Pamoja na kupeleka Umeme wa REA kwa Wananchi ambao bado hawajafikiwa, Kuunganisha Kata ya Mwansenkwa na Isyesye kwa Barabara ya Lami, Kuboresha Miundombinu ya Elimu na Kuhakikisha Wananchi wengi wananufaika na Mikopo inayotolewa na Halmashauri huku akiwataka kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura Wagombea wa CCM 29 Oktoba 2025.
 
 
 
Kampeni za Jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya “Uyole Kazi” ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi
 

									 
					