Leo 05 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbarali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Bahati Keneth Ndingo, ameendelea na kampeni zake za kishindo kwa kufanya ziara kubwa ya kampeni katika Kata ya Mahongole, akiinadi Ilani ya CCM kwa mwaka 2025.
Mhe. Bahati Ndingo amepokelewa kwa shangwe na mamia ya wanachama na wapenzi wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya Kata ya Mahongole, hususan katika eneo la Igalako, ambako wananchi wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza na sera za mgombea huyo
Katika ziara hiyo, Mhe. Bahati Ndingo alipata nafasi ya kutembelea maeneo ya biashara, vijiwe vya bodaboda, pamoja na vilabu vya pombe ambapo amezungumza nao moja kwa moja na wananchi kutoka vitongoji na vijiji mbalimbali vya kata hiyo, vikiwemo:
Mpakani, Kapyo, Nsonyanga, Mkoji, Ilongo, Ilaji, Mahongole, na Igalako.
Kata ya Mahongole ni kata ya 16 kutembelewa na Mhe. Bahati Ndingo tangu kuanza rasmi kwa kampeni zake za Kijiji kwa Kijiji, akiwa na lengo la kuomba kura kwa ajili ya ushindi wa kishindo wa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Kampeni hizi zinaongozwa na kaulimbiu ya “Tunaendeleza Tulipoishia – Mbarali Yetu, Fahari Yetu” Kauli mbiu hii ikiwa inalenga na kusisitiza Kazi, Maarifa, Nguvu, na kujituma zaidi kwa maendeleo ya wananchi.
Katika hotuba yake ya kufunga mkutano, Mhe. Bahati Ndingo aliwashukuru wananchi wa Kata ya Mahongole kwa kuwasihi kuwa wawe na imani na CCM huku akiahidi kuwa Chama hicho kitaendelea kuwa karibu na wananchi na kutatua changamoto zao kwa vitendo kupitia mipango imara ya maendeleo.
📲 Endelea kufuatilia taarifa na matukio ya kampeni ya Mhe. Bahati Keneth Ndingo kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii.
🔰 @Bahati Keneth Ndingo
#BKN #CCM2025 #MbaraliKwanza #MaendeleoKwaVitendo