Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilivyogundua Siri Ya Kuweka Bahati Yangu Kwenye Biashara Niliyoianza Kutokuwa Na Kila Kitu

January 10, 2026

Nilivyopata Mtoto Wa Kike Niliyemuhitaji Baada ya Miaka Ya Kutafuta Bila Mafanikio

January 10, 2026

Salama za Rambirambi kwenye Msiba wa Dada yake MNEC Ndele Mwaselela jijini Mbeya

January 10, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilivyogundua Siri Ya Kuweka Bahati Yangu Kwenye Biashara Niliyoianza Kutokuwa Na Kila Kitu
  • Nilivyopata Mtoto Wa Kike Niliyemuhitaji Baada ya Miaka Ya Kutafuta Bila Mafanikio
  • Salama za Rambirambi kwenye Msiba wa Dada yake MNEC Ndele Mwaselela jijini Mbeya
  • Nilivyorejesha Furaha ya Kuwa Baba Baada ya Watoto Kunikataa Kwa Muda Mrefu
  • Nilivyopata Amani ya Ndani Baada ya Kuacha Kuishi Kwa Kulinganisha Maisha Yangu na Wengine
  • Nilivyopata Amani Baada ya Miaka ya Kukosa Usingizi na Huzuni Usiku Kila Usiku
  • Nilivyopata Furaha Baada ya Kuachana na Marafiki Walionivuta Chini
  • Child Support Tanzania Yashirikiana na Madiwani Kuimarisha Elimu Jumuishi Mbeya
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAANZA RASMI KUTOA MAFUNZO YA HUDUMA ZA DHARURA KWA LENGO LA KUOKOA MAISHA NA KUPUNGUZA ATHARI ZA AJALI NA DHARURA ZA KIAFYA NYANDA ZA JUU KUSINI
Afya na Ustawi

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAANZA RASMI KUTOA MAFUNZO YA HUDUMA ZA DHARURA KWA LENGO LA KUOKOA MAISHA NA KUPUNGUZA ATHARI ZA AJALI NA DHARURA ZA KIAFYA NYANDA ZA JUU KUSINI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuNovember 26, 2025No Comments23 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeanza rasmi kutoa mafunzo ya magonjwa ya Dharura na Mahututi kwa watoa huduma za afya, wanafunzi wa kada za Afya pamoja Jamii Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kuokoa maisha na kupunguza athari za ajali na dharura za kiafya.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo leo tarehe 26 novemba,2025 katika kituo cha kutolea mafunzo hayo kwa vitendo kilichojengwa chini ya udhamini wa taasisi ya Abbott Fund, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema, kuanzishwa kwa mafunzo hayo kutasaidia upatikanaji wa wataalamu wenye weredi kwani kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wengi kuliko miundo mbinu ya kufundishia mafunzo haya kwa vitendo.

“…wote tunajua kwamba miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la wanafunzi kwenye vyuo vyetu ambalo haliendi sambamba na miundombinu ya kufundishia kwa vitendo.” – Dkt. Mbwanji

Aidha Dkt. Mbwanji ameishukuru taasisi ya Abbott Fund Tanzania, Wizara ya Afya pamoja (EMAT) kwa ushirikiano katika ujenzi wa kituo hicho cha kutolea mafunzo hayo.

“…lilianza kama wazo na sasa linaonekana hivyo niwashukuru sana Abbott Fund Tanzania, Wizara ya afya pamoja na (EMAT) kwa kuratibu upatikanaji wa kituo hiki”. – Dkt. Mbwanji

Kwa upande wake Dkt. Raya Mussa, Meneja Mradi huduma za dharura akiongea kwa niaba ya Taasisi ya Abbott Fund Tanzania ameishukuru Wizara ya Afya kupitia Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kukubali ujenzi wa kituo ambacho kitawanufaisha watoa huduma za afya, wanafunzi pamoja wataalamu wote wanapatikana Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika idara za Magonjwa ya Dharura na Ajali kutokana na miundombinu pamoja na vifaa ya kisasa vinavyopatikana katika kituo hicho.

“…lengo la kituo hiki si kunufaisha watu wa ndani tu lakini pia itanufaisha wanafunzi pamoja na watu wengine watakaohitaji kujifunza mafunzo haya hata kama si watoa huduma za afya”. – Dkt. Raya Mussa

Dkt. Prosper Bashaka ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema, maboresho ya upatikanaji wa huduma za dharura imekuwa ni kipaumbele kikubwa cha serikali, hivyo amewapongeza wadau wote walioshiriki katika jitihada za uanzishwaji wa kituo hicho cha kutolea mafunzo ya Magonjwa ya Dharura na Mahututi kwani kitaleta tija kwa hospitali na jamii hasa kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.

“…nitoe pongezi kwa wadau wote walioshiriki katika ujenzi wa kituo hiki kwani kitaleta tija kwa hospitali na zaidi wakazi wa Nyanda za Juu Kusini”. – Dkt. Prosper Bashaka.

Hadi sasa vituo hivyo vya kutolea mafunzo ya Magonjwa ya Dharura na Mahututi vimejengwa zaidi ya 6 nchi nzima kwa ushirikiano wa taasisi ya Abott Fund, Wizara ya Afya pamoja na EMART.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA APATA TUZO YA MWANAFUNZI BORA WA SHAHADA YA UZAMILI YA UDAKTARI WA MENO MUHAS.

December 8, 2025

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025

“Serikali yajizatiti kumaliza Fistula — Huduma bora kwa mama na mtoto yazidi kupewa kipaumbele”

May 21, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025297

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025239

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024213

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025132
Don't Miss
Uncategorized

Nilivyogundua Siri Ya Kuweka Bahati Yangu Kwenye Biashara Niliyoianza Kutokuwa Na Kila Kitu

By Mbeya YetuJanuary 10, 20260

Nilipoanza biashara yangu, kila kitu kilionekana kuwa kinyume nami. Hakukuwa na wateja, pesa ziliisha haraka,…

Nilivyopata Mtoto Wa Kike Niliyemuhitaji Baada ya Miaka Ya Kutafuta Bila Mafanikio

January 10, 2026

Salama za Rambirambi kwenye Msiba wa Dada yake MNEC Ndele Mwaselela jijini Mbeya

January 10, 2026

Nilivyorejesha Furaha ya Kuwa Baba Baada ya Watoto Kunikataa Kwa Muda Mrefu

January 9, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilivyogundua Siri Ya Kuweka Bahati Yangu Kwenye Biashara Niliyoianza Kutokuwa Na Kila Kitu

January 10, 2026

Nilivyopata Mtoto Wa Kike Niliyemuhitaji Baada ya Miaka Ya Kutafuta Bila Mafanikio

January 10, 2026

Salama za Rambirambi kwenye Msiba wa Dada yake MNEC Ndele Mwaselela jijini Mbeya

January 10, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025297

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025239

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024213
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.