Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI

December 29, 2025

Sikuweza Kulala Usiku Juu Ya Ndoto Mbaya Lakini Sasa Nalala Kama Mtoto Baada Ya Kupata Suluhisho

December 28, 2025

Nilihisi Kuna Kitu Kinazuia Maendeleo Yangu—Baada ya Kufunguliwa, Mambo Yalisonga

December 28, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI
  • Sikuweza Kulala Usiku Juu Ya Ndoto Mbaya Lakini Sasa Nalala Kama Mtoto Baada Ya Kupata Suluhisho
  • Nilihisi Kuna Kitu Kinazuia Maendeleo Yangu—Baada ya Kufunguliwa, Mambo Yalisonga
  • Baada ya miaka minane ya chuki familia yetu ilipata amani ndani ya siku nne tu
  • Baada ya siku za shaka nilifungua macho yangu na kugundua ukweli mchungu uliobadili kabisa mwelekeo wa ndoa yangu
  • Ndoa Yetu Ilikuwa Baridi Bila Mapigano, Mazungumzo Moja na Mtu Spesheli Yalifungua Mioyo Yetu
  • Nilijilaumu Kimya Kimya Kwa Mabadiliko ya Mwili Wangu Nilipoelewa Chanzo cha Ukavu, Afya Yangu Ilianza Kuimarika
  • Angalia watoto Kiwira Rungwe walivyo furahia sherehe ya Krismas kwa aina yake
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI
Habari za Kitaifa

NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuDecember 29, 2025Updated:December 29, 2025No Comments21 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC), Ndele Mwaselela, amewataka waandishi wa habari kuendelea kuzingatia maadili ya taaluma, kuandika habari za maendeleo na kuwasaidia wananchi kwa kuwaseemea, akisisitiza kuwa jamii inawategemea sana waandishi wa habari katika kusikika kwa sauti yao.

Mwaselela ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club), ambapo alizungumza na baadhi ya waandishi wa habari aliowakuta wakiendelea na majukumu yao ya kila siku ofisini hapo.

Akizungumza katika mazungumzo hayo ya ana kwa ana, Mwaselela alisema kuwa waandishi wa habari wana nafasi ya kipekee ya kuwa daraja kati ya Serikali na wananchi, kwa kuibua changamoto, mawazo na mahitaji ya wananchi kwa uwazi, usahihi na kwa kuzingatia misingi ya maadili ya uandishi wa habari.

“Wananchi wanawategemea sana waandishi wa habari kuwasaidia kuwasemea. Ni muhimu mkaandika habari zinazolenga kusaidia jamii, kuibua changamoto kwa njia ya kitaalamu na kuepuka uandishi wa habari unaochochea migogoro,” alisema Mwaselela.

Aliongeza kuwa pamoja na kuandika habari za maendeleo, waandishi wa habari wanapaswa kuepuka upendeleo wa aina yoyote, akisema kuwa uandishi usiozingatia misingi ya taaluma unaweza kuleta mpasuko na kutoelewana kati ya Serikali na wananchi.

Mwaselela aliwataka waandishi hao kuacha kuandika habari chonganishi, akibainisha kuwa vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kulinda amani, mshikamano na umoja wa taifa, huku vikichangia maendeleo kupitia uandishi wenye ukweli, uwajibikaji na uzalendo.

Aidha, alieleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta tofauti, hivyo ni jukumu la vyombo vya habari kuhabarisha jamii kuhusu jitihada hizo sambamba na kutoa nafasi kwa wananchi kueleza changamoto zao kwa njia yenye kujenga.

Kwa upande wake, Mwaselela ambaye pia ni mmiliki wa Shule za Sekondari za Patrick Mission na Paradise Mission, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi, vyombo vya habari na wananchi ili kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana.

Ziara hiyo ya kushtukiza ilihitimishwa kwa mazungumzo ya kirafiki na ya kujenga kati ya Mwaselela na waandishi wa habari aliowakuta ofisini hapo, ambapo walibadilishana mawazo kuhusu changamoto za uandishi wa habari na nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga jamii yenye amani na maendeleo.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MH. MAHUNDI AWAHIMIZA VIJANA KUISHI KWA MISINSI YA UWAJIBIKAJI NA UTU

December 23, 2025

DKT. TULIA ACKSON AANZA ZOEZI LA KUWAFIKIA KAYA ZENYE UHITAJI ZAIDI UYOLE, KAYA 130 ZANUFAIKA KUELEKEA SIKUKUU

December 21, 2025

MAHUNDI AWATUNUKU WAHITIMU 530 CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII(CDTI)UYOLE

December 20, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025275

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025238

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024212

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025131
Don't Miss
Habari za Kitaifa

NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI

By Mbeya YetuDecember 29, 202521

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC), Ndele Mwaselela, amewataka waandishi…

Sikuweza Kulala Usiku Juu Ya Ndoto Mbaya Lakini Sasa Nalala Kama Mtoto Baada Ya Kupata Suluhisho

December 28, 2025

Nilihisi Kuna Kitu Kinazuia Maendeleo Yangu—Baada ya Kufunguliwa, Mambo Yalisonga

December 28, 2025

Baada ya miaka minane ya chuki familia yetu ilipata amani ndani ya siku nne tu

December 27, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI

December 29, 2025

Sikuweza Kulala Usiku Juu Ya Ndoto Mbaya Lakini Sasa Nalala Kama Mtoto Baada Ya Kupata Suluhisho

December 28, 2025

Nilihisi Kuna Kitu Kinazuia Maendeleo Yangu—Baada ya Kufunguliwa, Mambo Yalisonga

December 28, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025275

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025238

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024212
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.