Leo, ujumbe kutoka benki ya NMB Makao Makuu Dar es Salaam, ukiongozwa na Hellen Lema Afisa Uhusiano na Ndugu Angumbwike Ngogo kutoka tawi la Mwanjelwa -Mbeya wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ziara iliolenga kuendeleza ushirikiano mzuri kati ya benki na hospitali, pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na huduma za kifedha na maendeleo ya mtu moja moja kifedha.
Bi. Hellen amepongeza Uongozi na Watumishi wa Hospitali kwa huduma nzuri za kibingwa na Bobezi wanaopatia watumishi benki hiyo na Watanzania pamoja na maboresho mazuri ya miundo mbinu ya kisasa ya kutolea huduma.
Amesema kuwa, Benki ya NMB inajivunia hospitali kuwa mshirika mkubwa kwa huduma zake kwa watumishi na hospitali hivyo kuahidi kuendeleza mahusiano hayo mazuri.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amewapongeza benki ya NMB kwa huduma bora wanazozitoa.
Ameonyesha kuridhishwa na ushirikiano wa benki hiyo katika kutoa huduma kwa hospitali na watumishi.
Aidha, amewahimiza wataalamu wa NMB kuendelea kuja kutoa elimu kuhusu fedha, uwekezaji, na ujasiriamali kwa watumishi wa hospitali, ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kuimarisha maisha ya wafanyakazi na wananchi wanaotumia huduma zao.

