Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASIHI WANAFUNZI TENGERU, KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

January 23, 2026

Aliiba Kila Siku Bila Kuonekana Siku Moja Hatua Moja Ilimrudisha Mwenyewe Akiwa Ametikisika

January 23, 2026

Nilianza Kudhoofika Bila Sababu Nilipogundua Nilikuwa Nachawiwa, Njia Hii Ilinilinda Milele

January 23, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASIHI WANAFUNZI TENGERU, KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII
  • Aliiba Kila Siku Bila Kuonekana Siku Moja Hatua Moja Ilimrudisha Mwenyewe Akiwa Ametikisika
  • Nilianza Kudhoofika Bila Sababu Nilipogundua Nilikuwa Nachawiwa, Njia Hii Ilinilinda Milele
  • Vibaka Wamvamia Mwandishi Rashid Mkwinda wa Mbeya Yetu Ajeruhiwa Vibaya Kichwani na Kulazwa
  • Boss Amtesa Mfanyikazi Bila Kujua Ndiye Mke Anayetakiwa Kumuoa, Yaliyojiri Ni Haya
  • Mama Wa Kambo Apata Usaidizi Wa Kudumu Baada Ya Kupata Mateso Kutoka Kwa Mabinti Wakorofi
  • Nyota Yangu Ilibiwa na Rafiki Yangu Wa Karibu Lakini Nilipata Mtaalam Aliyerejesha Kila Kitu Nilichopoteza
  • Alinitumia Uchawi Mbaya Nilijaribu Kujilinda Lakini Nilishindwa, Nilihisi Hakuna Njia Suluhisho Hili Lilirudisha Amani Yangu
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASIHI WANAFUNZI TENGERU, KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII
Habari za Kitaifa

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASIHI WANAFUNZI TENGERU, KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJanuary 23, 2026No Comments3 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ametembelea Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru mkoani Arusha na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa chuoni hapo, ikiwemo ujenzi wa jengo la Utawala, kituo cha uhifadhi wa machapisho yanayohusu wanawake, mabweni ya wanafunzi pamoja na Kituo cha Ubunifu wa Kidigitali na Huduma Tandaa (JODIC).

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala, Mhe. Mahundi amesema serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya vyuo vya maendeleo ya jamii ili kuimarisha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, sambamba na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.

“Miradi inayoletwa hapa chuoni inapaswa kusimamiwa kwa viwango vinavyokubalika ili thamani ya fedha itumike ipasavyo na kwa ubora unaostahili kwa manufaa ya wanafunzi na taasisi kwa ujumla,” amesema Mhe. Mahundi.

Aidha , Mhe. Mahundi amepata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa taasisi hiyo ambapo amewahimiza kutumia elimu wanayoipata chuoni hapo kwenda kuitumikia jamii kwa vitendo kwa kuwa elimu ya maendeleo ya jamii inapaswa kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii na siyo kubaki darasani pekee.

Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Dkt. Bakari George, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

“Hili jengo la Utawala na miradi mingine inaongeza ufanisi wa kiutendaji na kuboresha huduma kwa wanafunzi, Uwekezaji huu unaofanywa na serikali ni kielelezo cha dhamira yake ya kuimarisha elimu ya maendeleo ya jamii nchini,” amesema Dkt. George.

Ziara hiyo ya Naibu Waziri Mahundi katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imekuwa sehemu ya juhudi za serikali katika kuimarisha elimu ya maendeleo ya jamii nchini, kwa lengo la kuhakikisha vyuo vinaendelea kuzalisha wataalamu wenye ujuzi, ubunifu na maadili watakaotumia elimu yao kutatua changamoto za kijamii, kuendeleza ustawi wa wananchi na kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.

Na Jackline Minja – MJJWMM Arusha

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Child Support Tanzania Yawawezesha Madiwani Mbeya Kuhusu Elimu Jumuishi

January 8, 2026

NMB Yaimarisha Ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya

January 7, 2026

MHE. MAHUNDI AWASISITIZA WATOTO WA SHULE YA MAADILISHO IRAMBO KUBADILIKA NA KUJENGA MUSTAKABALI MWEMA

January 6, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025309

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025244

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024219

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025136
Don't Miss
Habari za Kitaifa

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASIHI WANAFUNZI TENGERU, KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

By Mbeya YetuJanuary 23, 20263

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi,…

Aliiba Kila Siku Bila Kuonekana Siku Moja Hatua Moja Ilimrudisha Mwenyewe Akiwa Ametikisika

January 23, 2026

Nilianza Kudhoofika Bila Sababu Nilipogundua Nilikuwa Nachawiwa, Njia Hii Ilinilinda Milele

January 23, 2026

Vibaka Wamvamia Mwandishi Rashid Mkwinda wa Mbeya Yetu Ajeruhiwa Vibaya Kichwani na Kulazwa

January 22, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASIHI WANAFUNZI TENGERU, KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

January 23, 2026

Aliiba Kila Siku Bila Kuonekana Siku Moja Hatua Moja Ilimrudisha Mwenyewe Akiwa Ametikisika

January 23, 2026

Nilianza Kudhoofika Bila Sababu Nilipogundua Nilikuwa Nachawiwa, Njia Hii Ilinilinda Milele

January 23, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025309

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025244

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024219
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.