Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA

February 22, 2026

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

February 22, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA
  • MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO
  • NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.
  • DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI
  • TAZAMA DKT TULIA NA DKT. MARY MWANJELWA WAKIIMBA WIMBO WA Umbili
  • UTANI WA DKT. TULIA ACKSON WAACHA HISIA NZITO MAZISHI YA MWANAHABARI MKONGWE ULIMBOKA MWAKILILI
  • MAHUNDI ASEMA SERIKALI INAWATHAMINI WAZEE KAMA HAZINA YA HEKIMA NA MAADILI YA TAIFA
  • SUMA FYANDOMO MGENI RASMI BARAZA LA WANAWAKE (UWT) RUNGWE AWASHUKURU KWA MSHIKAMANO
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA
Habari za Kitaifa

INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuFebruary 22, 2026No Comments4 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza leo Februari 22, 2026 na washiriki wa mafunzo ya makarani waongozaji wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Peramiho unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Februari, 2026. 
Na Waandishi wetu, Ruvuma na Songwe
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
imewataka Makarani Waongozaji wapiga kura katika Jimbo la Peramiho lililopo
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kutekeleza majukumu yao bila woga
kwa kufuata Sheria, Kanuni, maelekezo ya Tume.

 

Wito huo umetolewa na  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 22, 2026 wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya makarani waongozaji wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Peramiho unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Februari, 2026. 
 
“Nawasihi mnapokwenda kufanya kazi yenu mkawe wakarimu na wanyenyekevu katika kutekeleza shughuli zenu… .” amesema Jaji Mwambegele.
 
Jaji Mwambegele amewataka washiriki hao kutoa kipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalum wakiwemo watu wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokwenda na watoto wao vituoni.
 
“Jambo lingine nawasihi mkatende kazi yenu bila kumuogopa mtu yeyote bali mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume,” amesema Mhe. Jaji Mwambegele.

 

 

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku moja kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura klatika Jimbo la Peramiho 

 

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku moja kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura klatika Jimbo la Peramiho 

 

Katika hatua nyingine Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Asina Omari leo tarege 22 Februari, 2026 ametembelea mafunzo ya Makarani Waongozaji Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Shiwinga, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.

Mhe. Asina amewataka washiriki wa mafunzo hayo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume kwani wao ndio taswira ya Tume katika kufanikisha uchaguzi huo.

Amesema pamoja na jukumu lao la kuwaongoza wapiga kura kutekeleza haki yao ya kupiga kura kwa urahisi, wanapaswa kutoa elimu ya mpiga kura kwa wapiga kura ambao hawatambui utaratibu wa kupiga kura kituoni.

“Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yenu. Hivyo, niwakumbushe mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume” amesema Mhe. Asina na kuongeza….

“Kabla ya mafunzo mmeapa, viapo vyenu maana yake ni kwenda kutekeleza majukumu kwa uadilifu na kuzingatia weledi na kazi yenu ni zaidi ya kuwaongoza wapiga kura kwani mna jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura”

Amesema katika kutekeleza majukumu yao wanapaswa kushirikiana na watendaji wa uchaguzi na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ili kuhakikisha wanatatua changamoto wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Akifungua mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbozi, Ndg. Danny Tweve amewakumbusha washiriki hao kuwa wamechaguliwa kutekeleza jukumu hilo la kitaifa kwa niaba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hivyo, wanapaswa kutoa huduma kwa wapiga kura kwa uaminifu na weledi mkubwa na kwa kuzingatia sheria za uchaguzi ili kufanikisha uchaguzi huo na kuwasaidia wapiga kura kutekeleza haki yao bila usumbufu.

Uchaguzi katika Jimbo la Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma na Udiwani katika Kata ya Shiwinga, Halmashauri ya Mbozi Mkoani Songwe umeapangwa kufanyika Februari 26,2026.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku moja kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika Kata ya Shiwinga. 

 

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku moja kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika Kata ya Shiwinga. 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026

MAHUNDI ASEMA SERIKALI INAWATHAMINI WAZEE KAMA HAZINA YA HEKIMA NA MAADILI YA TAIFA

February 20, 2026

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

February 19, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025349

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024234

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss

INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA

By Mbeya YetuFebruary 22, 20264

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele…

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

February 22, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026

DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI

February 21, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA

February 22, 2026

MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO

February 22, 2026

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.

February 22, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025349

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024234
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.