Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato

February 25, 2026

WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI

February 25, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KUTOA WATAALAMU BORA

February 24, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato
  • WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI
  • SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KUTOA WATAALAMU BORA
  • INEC YAWAFUNDA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WA SAIDIZI WA VITUO VYA KURA JIMBO LA PERAMIHO
  • INEC YAWAPIGA MSASA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA PERAMIHO, SHIWINGA
  • MAHUNDI AONYA VIJANA KUTELEKEZA WAZAZI WAO
  • NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE, ASISITIZA UPENDO NA MATUNZO KWAKUWA WAZEE NI TUNU YA TAIFA.
  • DKT. MARY MWANJELWA ATOA USHUHUDA MZITO KWENYE MAZISHI YA ULIMBOKA MWAKILILI
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI
Habari za Kitaifa

WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuFebruary 25, 2026Updated:February 25, 2026No Comments2 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email
 Na Mwandishi wetu, Ruvuma
Wapiga Kura 127,632 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa kuchagua Mbunge katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma na Kata ya Shiwinga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Februari 25, 2026 mjini Songea Mkoani Ruvuma wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Februari 26, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 373 vya Kupigia Kura vitatumika.

“Kati yao wapiga kura 120,780 ni wa Jimbo la Peramiho na wapiga kura 6,852 wapo katika kata ya shiwinga na jumla ya vituo 373 vya Kupigia Kura vitatumika, ambapo vituo 354 vipo Jimbo la Peramiho na vituo 19 vipo katika Kata ya Shiwinga Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,”amesema Jaji Mwambegele.

Aidha, amesema kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Peramiho vyama vya siasa 15 vimesimamisha wagombea na  kwa upande wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Shiwinga vyama vya siasa nane (08) vimesimamisha  wagombea.

“Natumia fursa hii kuvikumbusha Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi kesho Februari 26, 2026 kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumlishia kura. Wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo na Kata husika, wamekamilisha taratibu zinazoweka mazingira yanayowawezesha mawakala wa vyama vya siasa kufuatilia mchakato mzima wa uchaguzi,”alisema Jaji Mwambegele.

Amesema, mawakala hao, wanawajibika katika kulinda maslahi ya vyama na wagombea wao. Hivyo, wanapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu za Uchaguzi na maelekezo ya Tume katika utekelezaji wa majukumu yao vituoni.

Jaji Mwambegele amesema vituo vitafunguliwa saa 01:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni na kwamba ifikapo muda wa kufunga kituo saa 10:00 kamili jioni, kama wapiga kura bado wapo kwenye mistari, mlinzi wa kituo atasimama nyuma ya mtu wa mwisho na zoezi la upigaji kura litaendelea hadi wapiga kura walio kwenye mstari watakapomalizika.

“Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kuondoka eneo la kituo cha kupigia kura; na Mpiga kura awapo kituoni, anatakiwa kufuata maelekezo yote atakayopewa na karani mwongozaji wapiga kura,”amesema Jaji Mwambegele.

Kwa mpiga kura ambaye ameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na taarifa zake zipo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililopo katika kituo husika, lakini amepoteza kadi yake au kadi yake imeharibika, ataruhusiwa kupiga Kura kwa kutumia moja wapo ya vitambulisho cha Taifa NIDA, Leseni ya udereva au Pasi ya kusafiria (Passport).

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato

February 25, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KUTOA WATAALAMU BORA

February 24, 2026

INEC YAWAFUNDA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WA SAIDIZI WA VITUO VYA KURA JIMBO LA PERAMIHO

February 23, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025354

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss
Habari za Kitaifa

Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato

By Mbeya YetuFebruary 25, 20263

Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato Mbeya-Katika hatua kubwa ya mapinduzi…

WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI

February 25, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KUTOA WATAALAMU BORA

February 24, 2026

INEC YAWAFUNDA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WA SAIDIZI WA VITUO VYA KURA JIMBO LA PERAMIHO

February 23, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Serikali na TNCC Kuunganisha Mifumo Kidigitali, TRA Yaimarisha Ukusanyaji Mapato

February 25, 2026

WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI

February 25, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KUTOA WATAALAMU BORA

February 24, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025354

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.