Author: Mbeya Yetu

Dkt. David Nassoro, Daktari Bingwa Mbobezi wa Mishipa ya Fahamu, amefafanua kuhusu magonjwa mawili yanayozua changamoto kubwa katika jamii – Kiharusi kinachowakumba zaidi watu wazima, na Degedege linaloathiri watoto wadogo.

Akieleza kwa undani, Dkt. Nassoro amesema Kiharusi hutokana na kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.

“Dalili za awali ni muhimu kuzitambua. Mgonjwa akipata ganzi upande mmoja, kushindwa kuongea au kuona, lazima apelekwe hospitali haraka – ndani ya saa tatu tuna nafasi kubwa ya kuokoa maisha,” amesema.

Kwa upande mwingine, Degedege limekuwa tatizo linalowachanganya wazazi, wengi wakidhani ni uchawi. Lakini Dkt. Nassoro amesisitiza kisayansi kuwa chanzo kikuu ni homa kali, hasa malaria.

“Wazazi wanapaswa kuelewa kuwa mtoto akianza kutetemeka, kupoteza fahamu kwa muda, au kuvuja mate, wanapaswa kumpeleka hospitalini mara moja. Kukaa nyumbani au kutegemea tiba zisizo sahihi kunaongeza hatari,” ameongeza.

Akihitimisha, Dkt. Nassoro amesema kinga ni hatua ya kwanza, ikiwemo kuzingatia lishe bora, kupunguza msongo wa mawazo, kufanya mazoezi, na kwa upande wa watoto kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na malaria.

“Elimu kwa jamii ndiyo tiba ya kwanza. Tukiepuka imani potofu na kuzingatia huduma za kitabibu, tunaweza kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania,” amesema Dkt. Nassoro.

Read More

Jina langu naitwa David kutokea Shinyanga, ni kijana wa miaka 28 ambaye nina nguvu kubwa ya ushawishi katika jamii yangu inayonizunguka hata katika mitandao ya kijamii ambapo nina wafuasi zaidi ya 200k. Ushawishi wangu kwa asilimia kubwa unatokana na mafanikio yangu na jinsi ambavyo nimekuwa nikiwasaidia watu katika shida mbalimbali ambazo zinawakabili. Hata hivyo, nisingeweza kuwa hapa nilipo bila ya msaada wa Kiwanga Doctors ambaye alisaidia kushinda mamilioni ya fedha katika jackpot ya bet ambayo nilicheza kwa mara kadhaa bila mafanikio. Kabla ya ushindi huo wa kushangaza, kazi yangu ilikuwa ni kufanya vibarua vya kuchunga ng’ombe za watu maeneo mbalimbali…

Read More