Author: Mbeya Yetu

Leo 05 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbarali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Bahati Keneth Ndingo, ameendelea na kampeni zake za kishindo kwa kufanya ziara kubwa ya kampeni katika Kata ya Mahongole, akiinadi Ilani ya CCM kwa mwaka 2025. Mhe. Bahati Ndingo amepokelewa kwa shangwe na mamia ya wanachama na wapenzi wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya Kata ya Mahongole, hususan katika eneo la Igalako, ambako wananchi wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza na sera za mgombea huyo Katika ziara hiyo, Mhe. Bahati Ndingo alipata nafasi ya kutembelea maeneo ya biashara, vijiwe vya bodaboda, pamoja na vilabu vya pombe…

Read More

Leo 04 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Tulia Ackson amesema kipaumbele kikubwa kwa sasa kwenye Sekta ya Afya Kata ya Mwansenkwa ni Kujenga Jengo la Mama na Mtoto pamoja na ukarabati wa Miundombinu kwenye Zahanati ya Kata hiyo. Akizungumza Mbele ya wakazi wa Mwansenkwa kwenye Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika Mtaa wa Luala Dkt. Tulia amesema akipata ridhaa ya kuwaongoza Wananchi wa Jimbo la Uyole atahakikisha Jengo hilo linajengwa ili huduma ya Mama na Mtoto ipatikane jirani tofauti na ilivyo sasa. Sambamba na hayo amesema ataendelea na zoezi la…

Read More

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Tulia Ackson amesema atahakikisha Wananchi wa Kata ya Mwakibete ambao hawajanufaika na Mradi wa REA wanafikiwa na Maradi huo ili kuondokana na Changamoto ya Kukosa Umeme. Akizungumza Kwenye Mkutano wa Kampeni zake eneo la Magaerejini Mtaa wa Viwandani Kata ya Mwakibete amewaeleza Wananchi hao kuwa asilimia kubwa ya Wananchi wa Jimbo la Uyole wamefikiwa na Umeme wa REA hivyo atajitahidi kufuatilia ili huduma hiyo iweze kuwafikia wakazi Wote huku akiutaja maradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kama suluhisho la Kudumu kukatika kwa Umeme. Katika hatua nyingine amewahakikishia…

Read More

Leo 29 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya CCM Dkt Tulia Ackson ameendela na Kampeni zake za kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Kata ya Ilemi ambapo amewahidi Wakazi wa eneo hilo Kuhakikisha Barabara ya Juhudi ambayo ni kero Kubwa kwa Wananchi inajengwa kwa Kiwango cha Lami kama ya Mapelele. Dkt. Tulia amesema wakati anaomba ridhaa ya kuliongoza Jimbo la Mbeya Mjini aliahidi Kujenga Barabara ya Mapelele ambayo tayari imekamilika, Pia aliahidi Ujenzi wa Barabara njia Nne ambayo Ujenzi wake unaendelea hivyo kwa sasa atahakikisha Barabara ya Juhudi na Ile ya kwenda Kituo cha Afya…

Read More

Leo 1 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya CCM Dkt Tulia Ackson amesema ahadi zinazotolewa na Chama cha Mapinduzi kwa Wananchi ni zauhakika kwani zimekuwa zikitekelezeka kwa uhakika kutokana na Msimamizi Mzuri unaofanyika Chini ya Serikali inayoundwa na Chama hicho. Akizungumza na Wananchi Kwenye Mkutano wake wa Kampeni eneo la Makondeko Sokoni Dkt. Tulia amesema mifano ya Jambo hilo ipo wazi, wakati anaomba ridhaa ya kuliongoza Jimbo la Mbeya Mjini aliahidi kupatikana kwa hospital ya Wilaya Jambo ambalo limekamika kwa kupata hospitali ya Igawilo ambayo inavifaa na Wataalamu wa kutosha, pia CCM iliahidi Ujenzi wa…

Read More