Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- WAKAZI MTAA WA KATI SOWETO MBEYA WAINGIA MTAANI WAJITENGENEZEA BARABARA ILIYOHARIBIWA NA MVUA
- WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LINDI, MTWARA, RUVUMA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI
- MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA YAFUNGULIWA LEO
- DROO YA MASTA BATA YA BENKI YA NMB KUWAPELEKA WATEJA WAKE KULA BATA DUBAI
- Jinsi nilivyoweza kupata mchumba toka nchini Marekani
- MATAPELI CCM WABAINIKA,NI WALE WANAOPITA KUOMBA FEDHA BILA RIDHAA YA CHAMA,WATANGAZIWA KIAMA CHAO
- MH. MAHUNDI VIJANA TUACHE KUTUMIA MITANDAO VIBAYA
- Bosi wangu anang’ang’ania kuzaa mtoto na mke wangu!
Author: Mbeya Yetu
Mgogoro umeibuka baina ya Lucas Mbwiga na Aidan Msigwa Wawekezaji wawili wa machimbo ya dhahabu katika Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ambapo kila mmoja anadai kulimiliki kihalali eneo la Kisumain lililokuwa na leseni ya uchimbaji wa madini kwa jina la Daud Mwantavila ambalo linadaiwa kupangishwa kwa Lucas bila ridhaa ya familia huku Aidan Msigwa akidai kulinunua kisheria na kubadilisha umiliki wa leseni kutoka kwa Daud na kuja kwake tangu April 22,2024.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde Juma Z. Homera amefika Mlima Kawetele uliopolomoka Alfajiri ya Leo na Kusababisha Kufukiwa kwa Nyumba 20, Ng’ombe Wanne na Kuharibika kwa Miundombinu ya Shule ya Generation katika Mtaa wa Gombe Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Akizungumza baada Kuwasili eneo la Tukio RC Homera amekanusha Uvumi unaozagaa Mtandaoni ukidai Kuna Maafa katika tukio hilo ambapo amesema zaidi ya hivyo vilivyotajwa Aya ya Kwanza hakuna Madhara mengine Wala Maafa kama inavyoripotiwa na Baadhi ya Watu.
Aidha Homera ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya Tathimini juu ya Waathirika hasa wale wasio na Malazi ya Kulala wahakikishe wanapatiwa Sehemu hizo wakati huu ambao Serikali inaendelea kupambana kuhakikisha Hali inakuwa Sawa katika Maeneo hayo.
Pia amekiagiza Kitengo Cha Ardhi Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuacha kuwapimia Wananchi Viwanja eneo lenye Changamoto hasa ya Mkondo wa Maji kwa kufanya Kwao hivyo kutasababisha Matatizo kama hayo ambayo yangeweza kuzuilika.
Tukio hilo limetokea Alfajiri ya Kuamkia Leo ambapo chanzo Chake ni Mvua zinazoendelea Kunyesha Mfululizo na Matukio yanayofanana na haya yamekuwa yakitukia Mikoa Mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Arusha na Lindi.
Watu wawili jinsi ya kike wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wanadaiwa kuuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka sita kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa aliyeuawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na mwingine ni Ivon Tatizo Haonga(16) mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.
Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 30,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.
Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje ya duka lake lililopo mita hamsini kutoka nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Edith Swebe Machi 30,2024 ameshiriki katika kongamano la Pasaka la Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) wa Shule za Sekondari Mkoa wa Simiyu ambalo limefanyika katika shule ya Sekondari Itilima iliyopo Wilaya ya Itilima.
Kamanda Swebe alipata fursa ya kuongea na vijana hao wa UKWATA Mkoa wa Simiyu na kuwahasa kujiepusha na matumizi mabaya ya Mitandao ya kijamii kwa kuangalia picha zisizo na maadili kitendo ambacho kinaweza kusababishia madhara ya afya ya akili na badala yake watumie mitandao ya kijamii kwa lengo la kujifunza.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuopoa mwili wa mtu jinsi ya kiume daraja la mto Magege Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka thelathini na nane hadi arobaini.Akitoa taarifa eneo la tukio Askari wa zamu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Abdalah Sebombo amesema tukio limetokea majira ya saa mbili kasorobo asubuhi machi 30,2024.Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Maswe Japhet Mahinya amesema alipata taarifa kutoka kwa mwananchi naye baada ya kufika eneo la tukio na kitoa taarifa Polisi,Polisi walipofika waliona mwili ukiwa korongo la mto hivyo ikawalazimu kuwasilana na…
Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson imetoa msaada wa vyombo vya kuhubiria Msikiti wa Masjid Bi Fatma Nzovwe Jijini Mbeya.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Dkt Tulia Ackson Afisa Habari wa Taasisi hiyo Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kutekeleza ombi la Msikiti huo kwa Mbunge ambapo waliomba vipaza sauti kwa ajili ya ibada.
Kwa niaba ya Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya msemaji wake Shekhe Ibrahim Bombo mbali ya kushukuru amewaomba waumini kumuombea dua ya heri huku akitaka vyombo hivyo vitunzwe kwa uangalifu.
Naye Hemed Kipengele kwa niaba ya Waumini ametoa neno la shukurani akimshukuru Mbunge kwa kutoa vifaa hivyo bila kujali itikadi za Kidini.
Aidha Justin Kayuni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ndanyela ameipongeza Taasisi ya Tulia Trust kwa kutoa vifaa hivyo kwani vitasaidia kueneza neno la Mungu.
Hatimaye Abdalah Yundu Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ameongoza dua ya kumuombea Dkt Tulia Ackson katika kazi zake za kila siku.
Dkt Tulia amekuwa akitoa misaada mbalimbali bila kujali itikadi za Kidini na Kisiasa ambapo hivi karibuni amefanikisha ujenzi wa Misikiti ya Tukuyu Mjini,Kiwira Wilayani Rungwe na Uyole Jijini Mbeya.
Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson imetoa msaada wa vyombo vya kuhubiria Msikiti wa Masjid Bi Fatma Nzovwe Jijini Mbeya.Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Dkt Tulia Ackson Afisa Habari wa Taasisi hiyo Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kutekeleza ombi la Msikiti huo kwa Mbunge ambapo waliomba vipaza sauti kwa ajili ya ibada.Kwa niaba ya Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya msemaji wake Shekhe Ibrahim Bombo mbali ya kushukuru amewaomba waumini kumuombea dua ya heri huku akitaka…
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutokea mkoa wa Mbeya Charles Mwakipesile amewajia juu baadhi ya watu hususani wapinzani ambao wamekuwa wakitoa maneno ya kejeli dhidi ya maendeleo yaliyoletwa na Rais Samia kwa kipindi cha miaka mitatu tangu achukue kijiti cha kuliongoza Taifa kutoka kwa Rais wa awamu ya tano aliyefariki dunia Dkt John Magufuli.
Timida Mpoki Fyandomo Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Mbeya ameahidi kutoa godoro kwa mjane Singwava Mwanyanje mwenye watoto sita mkazi wa Itanji Kata ya Iganjo Jijini Mbeya anayejengewa nyumba na Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini.Clemence Mwandemba Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mbeya amesema Dkt Tulia amekuwa akifanya mambo makubwa nchini kwa kuwagusa watu wenye uhitaji.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Itanji Javin Shaha amesema mama huyo anapitia kipindi kigumu hivyo anahitaji…