Author: Mbeya Yetu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amechangia shilingi milioni kumi kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Sokoine ikiwa ni utekelezaji wa agizo la TFF.

Katibu Mwenezi na Siasa Mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile amemshukuru Mwalunenge kwa hatua alizozichukua vinginevyo uwanja ungefungiwa.

Aidha Meneja wa Bens inayosambaza mbolea Israel Mwampondele ambao ni wadhamini wa Tanzania Prisons amesema uwanja utakarabatiwa uzio,jukwaa kuu na uwanja wa kuchezea mpira wa miguu.

Meneja wa uwanja Modestus Mwaluka amepongeza juhudi zinazofanywa na viongozi ili kuuboresha uwanja wa Sokoine.

Read More

#mbeyayetutv
MBUNGE KINANASI AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA WA MPIRA WILAYANI KYELA
Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Jumbe Kinanasi ameahidi kujenga uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu na shughuli mbalimbali za kijamii Wilayani Kyela.

Ameyasema hayo wakati wa kilele cha mashindano ya kuwania Kombe la Samia Maridhiano Cup yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano ya Amani Tanzania JMAT yaliyozikutanisha timu za Kasala Fc na Iteya FC ambapo timu ya Kasala ilishinda kwa jumla ya magoli 3-1 na kujitwalia Kombe na kitita cha Shilingi Laki Nane ambapo mshindi wa pili Iteya FC alijinyakulia kiasi cha Shilingi Laki Tano wakati viongozi wa Jumuiya hiyo walipozindua kombe la michuano hiyo wilayani Kyela.

Read More

#mbeyayetutv
RAIS SAMIA AMEONDOSHA VIKWAZO,MAANDAMANO NA MIKUTANO YA KISASA ITALETA MARIDHIANO KWA WANASIASA JMAT

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano ya Amani Tanzania JMAT Dkt Sheikh Alhad Mussa Salum amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameleta maridhiano ya kisiasa yaliyoondoa vikwazo vya kisiasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na kuvifanya vyama vya kisiasa kuwa na Uhuru wa kufanya siasa kwa kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa jambo ambalo halikuwepo hapo awali.

Sheikh Alhad amesema hayo wilayani Rungwe wakati alipokutana na baadhi ya wananchi katika muendelezo wa Maridhiano Day ambayo inawahusisha viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini na viongozi wa kimila ambayo yamefanyika kitaifa Jijini Mbeya.

Read More

Wazee wadau wa maendeleo mkoani Mbeya leo wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda na kujionea hali bora ya utoaji huduma. Wazee hao wameridhishwa na hatua za maendeleo zilizofikiwa na hospitali hiyo na wametoa sifa kwa uongozi wa hospitali kwa kazi kubwa wanayofanya.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo. Wazee hao walishuhudia usafi wa hali ya juu, upatikanaji wa vifaa tiba, na huduma bora zinazotolewa kwa wagonjwa.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, mmoja wa wazee alisema wamefurahishwa na maendeleo waliyoona na wanatambua juhudi zinazofanywa na wafanyakazi wa afya katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Hata hivyo, wazee hao wametoa wito kwa serikali na wadau kuhakikisha hospitali hiyo inapata fedha za kutosha ili kuendeleza maendeleo hayo.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imepokea sifa nyingi kutoka kwa wazee hao na imewasisitizia wananchi kuchukua tahadhari na kutembelea vituo vya afya mara kwa mara kwa ajili ya ukaguzi wa afya zao. Wazee hao pia wameahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa wazee hao, hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inaendelea kufanya maendeleo makubwa katika utoaji huduma za afya na wana matumaini makubwa kwa mustakabali wa sekta ya afya mkoani humo.

Read More

Jeshi la Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini katika kuhakikisha linaboresha huduma bora kwa Wananchi limeendelea kuwatambua na kuwapongeza Askari wa Jeshi hilo wanaofanya kazi vizuri zaidi ya kuhudumia wananchi sambamba na kuzuia uhalifu. Akitoa vyeti vya Pongezi kwa Askari hao leo Machi 01, 2024 katika bwalo la maafisa wa Polisi Arusha, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Utawala na Uchumi Bwana Daniel Luloku pamoja na kuwapongeza Askari waliofanya vizuri zaidi amewataka kwenda kufanya kazi kwa nidhamu na kwa weledi mkubwa ilikuhakikisha raia na mali zao wanabaki kuwa salama wakati wote. Bwana Daniel amewataka Askari wengine kuiga mfano…

Read More

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 2 Machi, 2024 ameshiriki katika Jopo la kujadili “Jukumu la Mabunge katika kuendeleza amani na maendeleo Duniani” ambalo ni sehemu ya Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya ulioanza jana tarehe 1 Machi 2024 kwa kufunguliwa na Mhe. Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.

Dkt. Tulia aliongoza sehemu ya majadiliano hayo na kuelezea namna Bunge linavyoendelea kuchagiza amani na demokrasia nchini Tanzania pamoja na Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unavyoendelea kutafuta suluhu na amani kwa Wanachama wake wakiwamo Urusi na Ukraine, Israel na Palestina, Azerbaijan na Armenia na wengine ambao wapo katika migogoro ya kukosa amani.

Mkutano huu unatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 3 Machi, 2024 Jijini Antalya, Uturuki.

Read More

Maadhimisho ya siku ya usikivu Duniani yameadhimishwa Kitaifa Mkoani Mbeya mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliyewakilishwa na Dkt Maisara Karume maadhimisho yalifofanyika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Katika hotuba yake Dkt Maisara Karume amesema takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa tatizo la usikivu ni kubwa na baadhi ya mikoa wanawake wanaongoza kwa tatizo la usikivu.

Dkt Maisara ameagiza hospitali zote za Rufaa za mikoa nchini kuwa na vifaa kwa ajili kubaini changamoto ya usikivu kwa wananchi.

Rais wa Jumuia ya Wataalamu wa masikio,pua na koo Tanzania Dkt Edwin Liyombo ameishukuru serikali kwa kuongeza wataalamu na vifaa katika hospitali nyingi nchini.

Naye Amina Mfaki mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali sanjari na kutoa elimu kwenye jamili ili kupunguza tatizo la usikivu kwa wananchi.

Taarifa imesomwa na Raphael Gabriel Katibu wa Jumuia ya wataalamu wa masikio pua na koo ikionesha Jumuia ina wataalamu zaidi ya mia moja ishirini wa kada mbalimbsli ambao walihusika kutoa huduma za afya,uchunguzi na utabibu katika wiki ya maadhimisho.

Dkt Benedict Ngunyale ni Daktari Bingwa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya mkuu wa kiitengo cha masikio,pua na koo amesema katika wiki ya maadhimisho wamezifikia shule kumi na moja za msingi na zaidi ya wanafunzi elfu tatu wamepatiwa elimu na uchunguzi wa masikio na matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt
Godlove Mbwanji amesema changamoto nyingi za usikivu zinasababishwa na upigaji wa muziki kwa sauti ya juu mathalani kwenye huduma za vinyozi ambazo huathiri pia wateja.

Mwinyi Kondo kutoka Wizara ya Afya ameomba vyombo vya habari kutoa nafasi kwa waataalamu kutoa elimu kwenye jamii.

Kupitia maadhimisho haya mbali ya wananchi kunufaika na elimu kutoka kwa wataalamu wa wananchi wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu bure.

Read More

Jumuia ya watumia maji ngazi 60 wamejitokeza kupanda miti zaidi ya 2000 chanzo cha Nzovwe 2 lengo kwa mwaka huu ni kupanda miti 10000 ili kutunza vyanzo mbalimbali Jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Vulustan David amesema zoezi hilo ni endelevu.

Kwa upande wake Mratibu wa Jumuia ya watumia maji bonde la Ziwa Rukwa Rhoda Mwinuka amewataka wananchi waofanya shughuli za kibinadamu ambazo ni pamoja na kilimo kuacha mara moja kabla hawajachuliwa hatua za kisheria.

Mwenyekiti wa mtaa wa Bomba mbili Kata ya Mwakibete amesema mpsngo huo ni endelevu ili kutunza vyanzo vya maji.

Read More