Author: Mbeya Yetu

Na Mwandishi `Maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa maono yake ya mbali na uamuzi wa busara wa kumpendekeza Profesa Mohamed Yakub Janabi kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaja hatua hiyo ya Rais Samia kama ishara ya kujiamini kama taifa, na uthibitisho kuwa Watanzania wanao uwezo wa kushika nafasi nyeti katika taasisi kubwa za kimataifa, wakielezea faraja yao kwa jinsi Tanzania inavyozidi kung’ara kwenye majukwaa ya kidiplomasia duniani. Aidha, Rais Samia amesifiwa kwa kuunda kikosi kazi maalum kilichoongozwa na Rais…

Read More

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali kutoka Wilayani Mafia mkoani Pwani  akimuonesha Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele orodha yawatu wasio stahili kuwepo kwenye Daftari.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitazama Mwandikishaji Msaidizi katika Kituo cha Kata ya Kilindoni kilichopo Shule ya Msingi Kilimani akichukua taarifa za watu waliopoteza sifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali wakati Mwenyekiti wa Tume alipotembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025…

Read More

Na Woinde Shizza, Arusha Serikali imepiga kengele ya tahadhari kufuatia ongezeko la madai feki ya bima yanayodaiwa kuisababishia nchi hasara ya mabilioni, huku ikiweka wazi kuwa asilimia 10 hadi 15 ya madai hayo duniani yana chembechembe za udanganyifu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Sada Mkuya, amesema hali hiyo imeifanya sekta ya bima kupoteza uaminifu wa umma na kuathiri utoaji wa huduma kwa wateja wa kweli wanaohitaji msaada halali. Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, wakati wa mkutano wa wataalamu wa udhibiti wa udanganyifu wa bima (IASIU), Dk. Sada alisema baadhi…

Read More

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati alipotembelea mafunzo ya siku moja ya watendaji hao ambayo yanahusisha waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kutoka Kata zote za Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani. Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.…

Read More