Author: Mbeya Yetu

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema kuwa Wizara inaendelea kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na vitendo vya utapeli mtandaoni, hasa vinavyofanyika kupitia huduma za simu na miamala ya kifedha (SimBanking). Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Fakharia Shomari Khamisi (Mb.), katika kikao cha Bunge kilichofanyika jijini Dodoma, Mhandisi Mahundi alisema ongezeko la matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) limeleta manufaa makubwa kwa taifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa, huku pia likizua changamoto mbalimbali ikiwemo uhalifu wa mtandaoni. Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka…

Read More

Lusaka, Zambia – Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule, amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, waliofika Ubalozini leo tarehe 12 Mei, 2025 asubuhi kwa ajili ya kujitambulisha. Wataalamu hao wapo nchini Zambia kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa Hospitali ya Kufundishia ya Zambia (University Teaching Hospital – UTH) kuhusu huduma ya uchujaji wa damu kwa njia tumbo (Peritoneal Dialysis). Katika mazungumzo yake na ujumbe huo Mhe. Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule aliwakaribisha wataalamu hao waliobeba bendera ya Tanzania, akisema kuwa ni…

Read More

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo Mei 12, 2025 ambapo Tume imetangaza kugawanywa kwa majimbo na kubadilisha majimbo. Na. Mwandishi Wetu, Dodoma Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema Tume imefikia uamuzi huo…

Read More

Maadhimisho ya Siku ya Msichana katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ndaki ya Mbeya, yalifanyika kwa mafanikio tarehe 10 Mei 2025. Hafla hii ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mheshimiwa Maryprisca Mahundi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF).

Katika hotuba yake, Mh. Mahundi aliwasihi wasichana wa chuo kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuathiri mustakabali wao, akisisitiza umuhimu wa elimu kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi na kijamii. Rasi wa Ndaki ya Mbeya, Prof. Henry Mollel, alishiriki pia na kupongeza waandaaji, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza maadhimisho haya kila mwaka.

Hafla hiyo ilijumuisha vipindi vya elimu, burudani, na majadiliano kuhusu nafasi ya msichana katika jamii. Mh. Mahundi aliahidi kuchangia shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike Ndaki ya Mbeya.

Siku hii huadhimishwa kila mwaka na Jumuiya ya Wasichana wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya kwa kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi (MUSO).

Read More

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kwa uongozi wake wa mfano unaoleta mageuzi chanya kupitia Mbeya Tulia Marathon.

Akizungumza Mei 10, 2025 katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya, mara baada ya kushiriki mbio fupi za Tulia Marathon, Mhe. Mahundi alisema kuwa mashindano hayo si tu ni burudani ya michezo bali pia ni jukwaa la kugusa maisha ya Watanzania wengi kupitia uboreshaji wa huduma za afya, elimu na kusaidia makundi yenye uhitaji.

“Spika Tulia si kiongozi tu wa kitaifa, bali ni dira ya matumaini kwa jamii. Kupitia Mbeya Tulia Marathon ameonyesha kuwa michezo ni daraja la maendeleo,” alisisitiza Mhe. Mahundi.

Mashindano haya yameendelea kuthibitisha kuwa michezo inaweza kuwa chachu ya mshikamano, afya bora, na maendeleo endelevu kwa taifa.

Read More