Author: Mbeya Yetu

Mashindano ya Riadha ya Betika Mbeya Tulia Marathon yametamatika leo kwa mafanikio makubwa katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya Mjini, yakiwashirikisha wanariadha zaidi ya 2,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania. Washiriki hao walichuana katika mbio fupi (za ndani ya uwanja) na mbio ndefu (Full Marathon), huku wakionesha viwango vya juu vya ushindani na nidhamu ya hali ya juu. Mgeni rasmi wa mashindano hayo alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, ambaye aliipongeza Taasisi ya Tulia Trust, chini ya uongozi mahiri wa Mkurugenzi wake ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Spika wa Bunge la Jamhuri…

Read More

Na Mwandishi Wetu, JAB Serikali imesema vitambulisho vya Uandishi wa Habari (Press Card), vitaanza kutolewa wakati wowote baada ya siku saba kuanzia leo Mei 3, 2025 baada ya Waandishi wa Habari kuanza kujisajili rasmi kwenye mfumo wa TAI-Habari. Mwandishi wa Habari ataanza kujisajili kupitia kiunganishi cha https://taihabari.jab.go.tz kisha kufuata maelekezo yaliyotolewa ili kukamilisha kujaza fomu yake kwenye mfumo huo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari. Kauli hiyo imetolewa tarehe 03 Mei, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, katika Kijiji cha Sayu mkoani Shinyanga wakati akizungumza…

Read More

Katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Comrade Kenani Kihongosi, alikabidhi cheti cha heshima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Zahara Muhidin Michuzi, kwa kutambua mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi. Bi. Zahara alihamishiwa wilayani Meatu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, akitokea Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara mkoani Morogoro, ambako pia alihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji huo. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Mji Geita katika Wilaya ya Geita, Mkoa…

Read More