Author: Mbeya Yetu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Mwaselela, amekabidhi vyerehani viwili kwa vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mbeya Mjini ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kuhamasisha uzalishaji wa ndani.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, MNEC Mwaselela alieleza kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya chama ya kujenga vijana waadilifu, wachapakazi na wenye kujitegemea. Alisisitiza kuwa uwezeshaji wa vitendea kazi ni kichocheo muhimu katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Viongozi wa UVCCM pamoja na wanachama walitoa shukrani kwa mchango huo na kuahidi kuvitumia vyerehani hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Read More

Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa. Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025 unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali.  Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo…

Read More

Mwemyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na watendaji wa uboreshaji ngazi ya Kata na Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Biometriki kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo Aprili 29,2025 wakati alipotembelea mafunzo hayo ikiwa ni maandalizi ya awamu ya pili mzunguko wa kwanza wa uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoanza Mei Mosi hadi Mei 07, 2025 katika mikoa 15. Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume. Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.   Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa…

Read More

Na Mwandishi Wetu, JAB Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua kadhaa katika kuimarisha na kuboresha sekta ya habari nchini ikiwa ni pamoja na kuunda Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari. Waziri Mkuu amesema hayo leo tarehe 29 Aprili, 2025 wakati akifunga Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Arusha kwa siku mbili. “Kwenye sekta ya habari na utangazaji, falsafa ya “4Rs” za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alizozibainisha baada ya kuingia madarakani mwezi Machi 2021, imetekelezwa kwa vitendo hususani kwenye…

Read More

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 29 Aprili 2025, amefungua rasmi Kongamano la Wasomi na Wanazuoni wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Spika amesisitiza umuhimu wa kulinda uhuru wa wanataaluma kama msingi wa maendeleo endelevu barani Afrika. Aidha, amewataka wanazuoni kutumia maarifa yao kuchochea mabadiliko chanya katika jamii. Kongamano hilo limeandaliwa na Ndaki ya Sayansi za Jamii ya UDSM kwa kushirikiana na Kanseli ya Maendeleo ya Utafiti katika Sayansi za Jamii (CODESRIA) na linatarajiwa…

Read More