Author: Mbeya Yetu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 18 Aprili 2025, ameongoza wananchi wa Jiji la Mbeya katika zoezi la upimaji na matibabu ya macho.

Zoezi hilo limeanza rasmi leo katika Shule ya Msingi Kagera, iliyopo Kata ya Ilomba na litadumu kwa siku tatu mfululizo. Huduma hiyo ya afya ya macho inatolewa bila malipo kupitia Taasisi ya Tulia Trust kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya.

Katika hotuba yake, Dkt. Tulia amewasihi wananchi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo muhimu kwa afya zao, akisisitiza dhamira ya Taasisi ya Tulia Trust katika kuboresha ustawi wa jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Read More

Rais Mstsaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiongozi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore mjini Ouagadougou na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili. Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

Read More

Mbeya, Tanzania – Aprili 2025
Wakazi wa maeneo ya Mwansekwa na Igodima jijini Mbeya wameeleza furaha yao kufuatia kuboreshwa kwa huduma ya upatikanaji wa maji safi katika maeneo yao, hali ambayo ni tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Wananchi hao wameipongeza Serikali pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA-UWSA) kwa juhudi walizozifanya kuhakikisha wanapata huduma ya maji kwa uhakika. Wamesema kuwa huduma hiyo imeleta unafuu mkubwa katika maisha yao ya kila siku, hasa kwa upande wa wanawake na watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.

“Kwa sasa tunapata maji karibu kabisa na nyumbani, tofauti na zamani tulipokuwa tukiteseka,” alisema mmoja wa wakazi wa Mwansekwa.

Kwa upande wake, MBEYA-UWSA imeeleza kuwa maboresho hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuboresha huduma za maji mijini na vijijini kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma hiyo muhimu kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Read More

Pembenzoni mwa Mkutano wa Uongozi wa Afrika wa nane jijini Kampala Uganda leo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kama mjumbe maalum, amewasilisha ujumbe maalum kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Rais Museveni alimshukuru kwa ziara na kumuomba amfikishie salamu zake kwa Mheshimiwa Rais Samia na watu wa Tanzania.

Read More