Author: Mbeya Yetu

Serikali mkoani Rukwa imekiri kuwepo uzembe katika usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa Vituo vya Afya Viwili na Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga,Mkoani Rukwa, yenye gharama ya shilingi Bilioni 2.6 ambayo imeshindwa kukamilika kama ilivyopanga lakini fedha zote zimekwisha.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA ameendelea na ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya, katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, ambapo imebainika matumizi ya fedha hayalingani na thamani ya fedha iliyotengwa na serikali.
Sendiga amesema mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mollo kilichotengewa shilingi Milioni 400 fedha zimekwisha majengo matano hayajakamilika, Kituo cha Afya cha Matanga kilichopelekewa shilingi Milioni 500 fedha zimeisha majengo hayajakamilika, Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga yua ISOFU iliyotumia shilingi Bilioni 1.8 majengo yake hayajakamilika.
Amesema kuna uzembe ambao umetumika kutekeleza miradi hiyo, na uzembe umejitoikeza katika usimamizi na ufuatiliaji, kwani utekelezaji wa miradi yote hiyo inakwenda kwa mfumo wa Force akaunti, Wananchi hawashirikishi katika utekelezaji wa miradi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga SEBASTIAN WARYUBA naye amekiri watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wamemuangusha kwasababu uzembe huo unawahusu, ikiwemo idara ya uhandisi, idara ya manunuzi na watendaji wengine.
Hata hivyo Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dokta IBRAHIMU ISAACK amebaini ukikwaji wa miongozo ya utekelezaji wa mfumo wa Force akaunti, ambapo ofisi ya manunuzi katika ofisi ya mkurugenzi iliwanunulia vifaa wananchi badala ya wajumbe wa kamati ya ujenzi wa vituo vya afya.
*********************MWISHO*******************

Read More

#MbeyaYetuTv
MUFTI ATUNUKIWA NISHANI MISRI

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeiry bi Ally akipokea toka kwa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi Tuzo ya Nishani ya Sayansi na Sanaa juzi huko Cairo baada ya kumalizika kwa hafla ya Maulid.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Awqaf Dkt. Muhammad Juma Mukhtar na Ahmad Twayb Sheikh Alazhar na mawaziri na mabalozi wa nchi mbali mbali na wanazuoni wakubwa wa Azhar Sharif pamoja na Mufti wa Misri DKt. shawqiy Allaam.

Mhe. Mufti amewa Nishani yeye na Waziri wa Awqaf kutoka Jordan Dr Muhamad Khalailah kwa kutambua mchango wao wa kuendeleza mafunzo ya Quran Tukufu, Uislama na Waislamu.

Read More