Author: Mbeya Yetu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amewashukuru watanzania kwa kuonyesha utulivu na uzalendo katika kuilinda amani ya Tanzania na kudumisha utulivu wakati nchi ikienda kuazimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara…..

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ukaguzi wa hali ya ulinzi na usalama katika mitaa mbalimbali ya jijini Dar es Salaam huku Vyombo vya Ulinzi na usalama vikiendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo tofauti nchini ambapo wananchi nao wametoa maoni yao.

Read More

Na WAF, Dar es Salaam.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kuwatibu watu 760 wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu ambapo shilingi Bilioni 6.7 zimetengwa kwa kazi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26

Hayo yameibainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa Desemba 8, 2025 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Sekta ya Afya ngazi ya Wizara waliopo mkoa wa Dar es Salaam kwenye kikao kazi kilichofanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Kutokana na faida kubwa iliyopatikana kwa mwaka 2024/25 ambapo jumla ya wagonjwa 677 walinufaika kwa huduma za kibobezi kama kupandikizwa Uloto watoto wenye Sikoseli, Kupandikizwa figo, upasuaji wa moyo, uapndikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto, matibabu ya Saratani, upandikizaji wa nyonga, Rais Samia ameridhia kuwa na bajeti husika,” amefafanua Waziri Mchengerwa.

Waziri Mchengerwa amesema Rais Samia anadhamira ya dhati ya kuboresha Afya za wananchi kwakuhakikisha kila mwananchi uhitaji wa huduma za kibingwa anapata huduma hizo pasipo na kikwazo cha fedha. @wizara_afyatz @mohamed_mchengerwa

Read More

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, katika Ikulu ya Chamwino, kujadili maeneo muhimu ya ushirikiano na kuimarisha dhamira ya pamoja ya kujenga ushirikiano wa kisasa na wenye manufaa kwa pande zote mbili. Balozi Lentz—aliyefuatana na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa na Uchumi—amesisitiza dhamira ya Washington kuhuisha mahusiano na kuongeza kina la ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya mataifa haya mawili. “Marekani imejitolea kujenga ushirikiano usiotegemea misaada, bali unaojengwa juu ya ustawi wa pamoja,” alisema Balozi Lentz. Mazungumzo yamejikita katika hatua…

Read More