Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Naibu Waziri Kundo: Mradi wa Maji Mto Kiwira Umefikia Asilimia 98
- Madaktari Walimwambia Ataishi na Maumivu Milele Lakini Ndani ya Miezi Sita Kila Kitu Kilibadilika
- Walimdharau Kwa Miaka Kwa Sababu ya Umaskini Leo Anasaini Contracts za Serikali Zenye Thamani ya Mabilioni
- This time I give steve a link (no mid-stream ads)
- What is Charlie Kirk’s Security Man Brian Harpole Twisting and Squeezing at the Big Bang? – #33
- Aliachwa na Mpenzi Wake Siku Moja Kabla ya Harusi Miezi Michache Baadaye Dunia Ilimshangaa
- BREAKING! MIT SCIENTIST SUSPECT MANHUNT , KASH INTERVIEW, TRUMP ADDRESS, NEWSOM & REAGAN, BLACK TV
- View the subsequent content through the homepage link#usa #shortsvideo #newyork
Author: Mbeya Yetu
Na Abel Paul,Jeshi la Polisi- Tinde Shinyanga.
Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo STPU Kimesema Kinawashikilia watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma za wizi wa mifugo na utoroshaji Mifugo nje ya nchi huku likisema kuwa litaendelea kushirikiana na wananchi kwa karibu ili kudhibiti uhalifu huo hapa nchini.
Akitoa taarifa hiyo leo Machi 12,2024 na kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua wakati alipotembelea mnada wa Tinde uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga amesema Jeshi hilo linawashirikilia watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.
Kamanda Pasua ameongeza kuwa watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za wizi wa mifugo katika maeneo tofauti hapa nchini majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi ambapo amesema kikosi hicho kitaendelea kuwakamata wale wote watakao bainika katika kujihusisha na wizi wa mifugo.
Aidha amewaomba wananchi kote nchini kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo Pamoja na kutorosha mifugo nje ya nchi.
Kwa upande wake afisa biashara Kutoka Shinyanga vijijini Upendo Milisho amebainisha kuwa wananchi na wafanya biashara mifugo katika mnada wa Tinde uliopo halmashauri ya Shinyanga wamekuwa na mwitikio Chanya katika ulipaji Ushuru kwa kielektroniki mnadani hapo.
Afisa Mapato Wilaya ya Shinyanga Bw. Victor Moleli Pamoja na kushukuru kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo amebainsha kuwa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi wameendelea kudhibiti uhalifu katika eneo hilo la mnada wa Tinde kitendo kilichopelekea mnada huo kuwa miongoni mwa minada yenye kukusanya mapato vizuri na usalama wa kutosha.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Taasisi ya 1 New Heart Tanzania inayojihusisha na upimaji wa moyo kwa watoto imewaka kambi ya siku tatu ya uchunguzi na upimaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Dkt. Nuru Mniwa Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema lengo la kambi hiyo ya siku tatu ni kutoa huduma ya uchunguzi na vipimo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 ili kutambua matatizo mbalimbali ya moyo yanayowakumba pamoja na kuwapuguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma hiyo.
“..changamoto kubwa ni uwezekano wa watoto hawa kufika Taasisi ya Moyo ya JKCI pale wanapobainika na tatizo la moyo kutokana na umbali na gharama za kujikimu”.- Dkt. Nuru Mniwa
Kwa upande wake Dkt. Gloria Mbwile, Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema, magonjwa ya moyo kwa watoto yamegawanyika katika makundi mawili ikwemo magonjwa ya kuzaliwa nayo pamoja na yale yanayoytokana na maambukizi.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia mwanamke Mkazi wa kijiji cha mashese wilaya ya Mbeya Mkoa wa kwa kuwaua wanawe wawili kwa sumu
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara…
MARIDHIANO DAY ILIVYOADHIMISHWA MBEYA,PROF MKENDA,ANNE MAKINDA,VIONGOZI WA DINI WALIVYOIELEZEA AMANI
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amewataka viongozi wa madhehebu ya kidini Nchini kuendekeza maridhiano ya amani ili kutunza amani na mshikamano uliopo katika Taifa.
Amezungumza hayo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maridhiano Jijini Mbeya alipomwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa Hotel ya Tughimbe.
Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo limesema litaendelea kutoa elimu kwa wafugaji na wafanya biashara wa Mifugo hapa Nchini huku likibainisha kuwa halitomwonea muhali mfugaji yeyote atakaye bainika kutorosha mifugo na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini. Hayo yamebainisha leo Machi 09, 2024 Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo hapa nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua alipotembelea mnada wa Upili Igunga ambapo amebainisha kuwa kikosi hicho kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji Nchi nzima ili kuondokana uvunjifu wa sheria. Wauza mifugo wa Mnada…
Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha
Ikiwa leo ni Machi 08,2024 kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, Mtaandao wa
Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha wameunga na wanawake wengine Mkoani humo huku
Mtandao huo wakiitumia siku hiyo kuwawekea akiba ya fedha katika mfuko wa uwekezaji (UTT)
kwa Watoto wawili wa askari wanandoa waliofariki kwa ajali ya gari.
Akiongea katika Viwanja vya Ngarenaro Complex Jijini Arusha Mwenyekiti wa Mtandao huo
Mkoa wa Arusha Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema mtaandao huo
katika kuelekea kilele hicho ulianza mapema kutoa elimu maeneo mbalimbali Pamoja na
kufanya ibada ya kuwaombea marehemu.
SSP Zauda ameongeza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo waliona vyema kuunga na
kuwawekea akiba ya fedha kwa Watoto wa askari wanandoa waliofariki katika ajali ya gari
ambapo amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia Watoto hao katika swala la elimu na
mahitaji mengine ya kibinadamu.
Aidha ametoa wito kwa wanawake wengine Mkoani humo kufanya kazi kwa bidii,nidhamu na
kutenda haki ili ustawi bora na wajikwamue kiuchumi na maendeleo ya Taifa kwa Ujumla.
Nae mrakibu msaidizi wa Polisi Lucy Teesa kutoka Makao Makuu ya kikosi cha Kuzuia wizi wa
Mifugo STPU amewaomba wanaweka wenzake kushiriki vyema katika mapambano dhidi
uhalifu ambapo amewaomba kutoa taarifa za uhalifu na kujikitaa katika malezi bora ya Watoto
ili kujenga Jamii iliyostarabika.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Murieti Mrakibu msaidizi wa Polisi
ASP Tausi Mbalamwezi amewaomba wanawake wenzake kujiamini na kujituma katika
kutekeleza majukumu yao huku akiwaomba kuumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliinua taifa kiuchumi.
Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amezidi kuyafikia makundi mbalimbali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi. Miongoni mwa kikundi kilichofikiwa na mkono wa kheri ni kikundi cha Mwanamke Shujaa cha Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambacho kimechangiwa shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya kufugia mifugo mbalimbali yeye akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kiwilaya Tukuyu mjini lengo ni kupata 20m kufanikisha malengo. MAHUNDI ACHANGIA 5M KIKUNDI CHA MWANAMKE SHUJAA RUNGWE Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum…
